MaKAVU LIVE PART 3

MaKAVU LIVE PART 3

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Posts
7,479
Reaction score
5,161
Mhh swala la usafi ni mtihani wandugu,

ANGALIZO: HII NI MAALUMU KWA WENYE TABIA HIZI TU NA SIO WOTE

Pamoja na kwamba siku hizi nguo za ndani kama braa na chupi zimejaa kariakoo, mchina alisharahisisha huduma kwa bei chee tu ya 1000 ushapata cotton yako japo ya low quality BADO inashangaza unakuta mdada mrembo kweli kweli, high hill zake, kiswanglish kwa sana tu na mapozi kibao anavaa chu***pi hadi inaota sugu za uchafu maeneo flani.. kwenye hanger amejaza mich*upi myeusi na hata zikiwepo nyeupe basi zimefubaa hadi aibu......(hii siongei bla bla nimeona kwa macho yangu kwa baadhi ya wadada tena wenye elimu zao (master na bachelor) na kazi zao za maana tu, ofisini wanaheshimika kweli kumbe usafi kwao 0) ........kwanza nani alikuambia ch*u*pi ya mwanamke ni nyeusi?? labda kwa mida flani tu unaweza kuwa na black lakini mwanamke shuti usafi na rangi nyeupe au pink ndio rangi za kike, rangi hizi ni kipimo halisi cha namna ulivyo msafi. Unakuta kinguo cha ndani kimevaliwa miaka nenda rudi hata hakibadilishwi?? Kwani hukufunzwa ulipokuwa mtu mzima (i.e. baada ya kuvunja kikombe) ??
Haya tena, utakuta kibraaa nacho kimechinaaaa utadhani kimefukizwa moshi na mvaaji ni mpishi wa mashuleni. Jitahidini walau, huduma zimerahisishwa na mchina siku hizi. Usafi sio foundation usoni na wanja....

WAKAKA: Unakuta mkaka handsome kweli kweli, amechomekea design, upanga wa surual ya kushona ndo usiseme....mdada unaona hapa nimepata wa ukweli. Sasa siku ya siku unamkaribisha kwako, mgeni shuti kuvua kiatu mlangoni, harufu inayotema hapo hata mood yote inaisha. Kumwambia huwezi, basi na yeye ndo amekazia kweli kuleta story zake as if ile harufu yeye haijaingia kwa pua zake. Unakuta socks inavaliwa wiki nzima na mijoto ya dar utadhani madukani zimeisha...... nunua pea hata 30 walau kila siku na socks zake, pia jaribu kuweka viatu vyako kwenye jua angalau kila wiki mara moja au mbili wakati wa week end. Kama unanuka miguu sababu ya ugonjwa basi jaribu kwenda hospitali mapema utibiwe. Wajameni eeh tujikague na kuweza kutambua harufu hizi ili zifanyiwe kazi mapema isiwe kero. Hata poda ya 500 tu ukiwa unaipaka miguuni ndio uvae socks then viatu inakata harufu yoote ya miguuni.

Na boxer zenu za kijani, brown na njano.....mhh sijui wengi wenu hamzifui? mkaka akivua tu nguo harufu hiyoooo mhhh kwakweli mnakatisha tamaa sana. mfano mzuri ni kule mabibo hostel ukiingia tu kwenye vyumba vya wakaka walio wengi (sio wote msije niparua) utakuta kunatema harufu flani kama mixer ya janaba na uvundo hivi. Najua wengi mtabisha ila ndo hivyo mie nshatoa yangu.

Hii ni kwa wanaume walio wengi wakubwa kwa wadogo. Mwanaume utabaki kujiuliza mbona mie kila nikitongoza sikubaliwi....kumbe mwenzako alichoka na hali kama hizo na hivyo mood yote ya kukukubali imemtoka. Ni jambo dogo ila lina madhara makubwa.

Hii inaitwa MAKAVU LIVE PART 3, Hutaki mi ndo nshayasema hivyo kama ngumu kumesa tafuta maji ya dasani ushushie.

MAMBO GANI HAYA KUFUNDISHANA USAFI UKUBWANI?
 
sijapTa ona sister ana maneno kama mwimba taarab
 
.....yan ndo umekuja kunisema mpaka huku Jamvini? but me love you bado mrembo...:A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2:
 
Nakunyatia nikukague nione kama huna kasoro hata moja hata mi-mbaa kichwani .........!:rockon:
 
we unavaa pichu kwa mda gani? ok!! sory kumbe hua unabeba ktk mkoba wakoule kwri uko smart bibie.. haya wazee wa boxer za kijana ujumbe tyr ndio huo
 
suala la usafi ni karama hata ufundishwe vp kama wewe ni mchafu utaendelea kuwa mchafu.
 
Yes most of the boys room zinanuka uvundo tena ukienda hizi boarding schools
utafurahi na harufu
 
mama yetu alikuwa anapiga marufuku kutoka bafuni na chupi kavu.......
kila ukitoka kuoga unapitia kwa mama kukagua kama chupi imetakata, ndo uende ukajipake mafuta na kuvaa.....
hiyo tabia haiwezi kunitoka maana niliianza nilipoanza kujiogesha tu, hata kama nitaoga mara 4 kwa siku basi nitabadilisha chupi mara 4 na zote zitakuwa zimefuliwa.....
Tuwafunze watoto wetu tabia za kujifulia nguo zao za ndani wanapooga..... wasije wakasubiri kwenda kufuliwa chupi na wake zao....
ref... https://www.jamiiforums.com/mahusia...yanayochangia-mume-kutembea-na-hausigeli.html
 
thawathawa mrembo by necha, nashukuru kwa kutukumbusha, nilijua nakosea kumbe niko sawa kwamba sina tabia ya kurudia nguo/viatu, i mean nafua shati zangu 7 na soksi(zipo nyingi, sikumbuki ni pair ngapi), viatu pea tano, weeknd raba......nashukuru Mungu kukupa kipaji cha kutukumbusha kwa sababu kuna watu hawajui hata kutandika.
 
Hii ni kwa wanaume walio wengi wakubwa kwa wadogo. Mwanaume utabaki kujiuliza mbona mie kila nikitongoza sikubaliwi....kumbe mwenzako alichoka na hali kama hizo na hivyo mood yote ya kukukubali imemtoka. Ni jambo dogo ila lina madhara makubwa.

Hii inaitwa MAKAVU LIVE PART 3, Hutaki mi ndo nshayasema hivyo kama ngumu kumesa tafuta maji ya dasani ushushie.

MAMBO GANI HAYA KUFUNDISHANA USAFI UKUBWANI?

Umenikumbusha room mate wangu ambaye alikuwa na tatizo 'sugu' la kikwapa nilipokuwa chuo. Kila akitongoza alikuwa hakubaliki kwa maana kiukwel jamaa alikuwa anatema. Akitoka kuoga ukipishana nae unatamani umuamrishe arudi bafuni. Nadhani pengine yeye alikuwa haisikii hiyo harufu.

You can't believe, kuna mdada mmoja alikuja 'kujitoa mhanga' akamkubali yule jamaa, haikupita mwezi jamaa alikuwa hatemi hata chembe ya harufu, kawa very handsome had wadada waliokuwa wanamcheka mwenzao mwanzoni wakaona wivu. Hadi sasa hawa ni mme na mke, na maisha yao yanaenda vyema...
 
Tuko hakuna kitu nakereka kama kuwa na mwanaume mnuka miguu, kweli Mungu anisamehe sana. Nishawakataa wengi sana tu baada ya kuliona hilo. Muda wa kuwekana chini kwenye utu uzima huu kufundishana ABC za usafi kweli ni ngumu. Ina maana yeye hajijui? mbona mimi siku kukiwa na harufu tofauti mwilini naigundua kirahisi tu? Yani saa ya kukutana ikifika unaumiza kichwa juu ya namna ya kukabiliana na harufu? hapana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom