Kundya Rajabu
Member
- Mar 22, 2018
- 7
- 0
Kumekuwa na vuta nikuvute ya wapi makao makuu ya halmashauri ya singida kaskazini yajengwe kati ya Ilongero na saga rumba. Kwa tabia ya wana singida kaskazini hili lisingekuwa tatizo kubwa wangepokea vyovyote vile.
Tatizo linakuja kwa kuwa wananchi wa Ilongero walishaaminishwa kuwa makao makuu yatakuwa ilongero.
Serikali kwa maana ya Mkuu wa Mkoa alikwenda kuwajulisha na akaagiza halmashauri ihamie huko, mapema halmashauri ilishaamua makao makuu yawe ilongero kabla ya kubadilika, CCM iliamua makao makuu yawe ilongero na wameshafungua ofisi ya wilaya, ofisi ya mbunge ipo ilongero.
Sasa unapowaambia watu makao makuu yanaenda sagarumba hawaelewi na hawataelewa. Jambo hili linafanywa ni rahisi lakini ni gumu maana Kwenye mioyo limeshapandizwa na chuki na mifarakano inaonekana japo wasiotaka kuona wanajifanya hawaoni.
Tatizo linabaki je watu kufarakana na kujenga chuki ni jambo dogo? Viongozi wa CCM na Serikali hasa ngazi ya mkoa lazima waketi pamoja haraka na kwa pamoja waende kuonana na Serikali kuu wakiwa na msimamo mmoja kisha warudi kukabiliana na wananchi.
Kujisikia, kujiona, hakupaswi kuwa sababu ya kupoteza upendo na msikamano baina ya wananchi na baina ya wananchi na Serikali yao.