Makamu wa raisi wa JMT Dk nani sijui yule (nimemsahau jina), yule mzee wa kizanzibar, yuko wapi? mzima wa afya? Mi nilidhani kwa kusafiri raisi yeye ndiye angeachiwa mikoba, lakini naona Pinda ndiye yuko responsible na kila kitu. Ameenda wapi huyu mzee?
Kukata utepe.Hivi anaitwa Dokta nani tena.... aaah jina lake gumu sanaaaa... aaah... J.K. aliwahi kumuita Shababi... hivi kazi yake ni nini hasa???
Huyu mwamba yupo kweli kitambo sana sijamsikiayupo anachunguza sehemu za kuchimba urenium maana si ni mtaalamu wa nyukilia pekee alayebaki baada ya tanzania kuogopa kumtumia kwa kuwaogopa wamarekani, sasa naona wameruhusu sijui naona harakari pale kwenye hifadhi, naogopa isije lipuka kama mbagara na ukonga, sijui nyie mwasemaje, mtaarumu mnamkimbizia kwenye siasa nchi itaendelea kweli? huyu mtaalam wa nyukilia leo hii yuko kwenye masherehe anatembea na mkasi kukata utepe!!!!