figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto amesema hapendezewi na tabia ya Jaji Mkuu wa nchi hiyo Willy Mutunga kuvaa hereni. Ruto alikuwa akijibu swali la mtangazaji wa kituo cha TV na akasema: "Sipendezwi na jambo hilo, mtoto wangu mdogo anasomea sheria ananiulizaga kuhusu kitendo hicho lakini nakosa majibu ya kumpa."
Baadhi ya watu wamekuwa wakimtetea Mutunga, wakisema uvaaji wa hereni ni sehemu ya utamaduni wa kiafrika.
Kumbuka huyu Jaji Mkuu alitoa hukumu ya maandamano ya CORD kuendelea, vilevile alishawahi kufungwa jela na inasemekana alifungwa gereza moja na Odinga kipindi cha Rais Moi wakati wa mapambano ya kudai vyama vingi, Hivyo ukaribu wao na Misimamo imara ya Jaji mkuu ambaye hateteleki bali anasimamia sheria, Hiyo inaweza kuwa unamkera Makamu wa rais Ruto