Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,439
- 6,692
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewasha Mwenge wa Uhuru kuashiria uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha mkoani Pwani leo tarehe 02 Aprili 2025.
Mpango amesema Serikali ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaendelea kusimamia kwa dhati na kwa haki misingi ya demokrasia na kuhakikisha wananchi wanatumia haki yao ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi kwa uhuru
Dkt. Mpango amesema hayo wakati akizindua Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha mkoani Pwani, akitoa wito kwa wananchi wote hususan vijana kuwa waangalifu na watu wasioitakia mema nchi kwa kuepuka kutumiwa vibaya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani.
Makamu wa Rais amesema Wadau wote wa uchaguzi, hususan vyama vya siasa wanahimizwa na kukumbushwa kuwa wana wajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika katika hali ya amani na utulivu
Ameongeza kwamba Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 42(2) na 65, Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya Mwaka 2024 pamoja na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Na. 4 ya mwaka 2018.