Kiazi Kitamu
Senior Member
- Feb 16, 2013
- 122
- 126
Mnamo tarehe 19.05.2023 Makamu wa Rais Dkt. Mpango uliweka Jiwe la msingi kwa ujenzi wa barabara kiwango cha lami Mianzini mpaka Ngaramtoni yenye urefu wa kilomita 18 Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.
Na kubwa ulituhaidi wananchi wa Kijiji cha Olemringaringa mpaka Ngaramtoni tutalipwa fidia mapema kabla ya bajaeti ya 2022/2023 au mapema sana mwezi Julai mwa bajeti ya 2023/2024 ila cha kusikitisha Sana [emoji24][emoji24] mpaka sasa hakuna cha fidia yoyote na mkandarasi yuko site ameshakamilisha madaraja.
Na mwisho mwa wiki Mkuu wa Wilaya ya Arumeru alituma Mwakilishi na kutoa maelekezo kuwa tupishe maeneo yetu na kuwa tutalipwa baadae kitu ambacho ni kinyume cha sheria ya Ardhi.
Je, Makamu wa Rais Dakta Mpango ulitudanganya au ulidanganywa?