Makamu wa Rais awasili Arusha

ng'ombo

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
418
Reaction score
619

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo Mhe. Makamu wa Rais ataongoza wananchi wa Arusha na Mikoa ya jirani kesho katika kuaga miili ya wanafunzi, waalimu na dereva waliofariki katika ajali ya bus la Shule jana.

Pichani ni muonekano wa majengo ya Shule ya Lucky Vicent katika matokeo ya darasa la 7 mwaka 2016 Shule hii ilishika nafasi ya kwanza kati ya Shule 331 Kimkoa na nafasi ya 20 kati ya Shule 8109 Kitaifa. Jambo lilofanya wazazi wengi kupeleka watoto wao katika Shule hii.
 
Wapumzike kwa amani marehemu wote.
 
makamu kapendezaa

Huyu Mama ni Hallat kwelikweli na ni Mjanja sana anajua kutupia hata Yule Binti yake ambae pia ni Mwakilishi kule Znz nae sio haba ana shawishi Washawishika Kama Mie!

Humkuti Katupia Mavitenge Kama Salma na Janet!

Sote tumefiliwa Ila wana Arusha wamefiliwa zaid![emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Mola Awape Faraja na subira Wafiwa !
 
ni jambo jema sana kuwasili kwake hasa kipindi hiki cha majonzi.
 
Amiiin ijapo nimechelea kukujib
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…