Makampuni ya simu kutozwa faini kwa kushindwa kufikisha huduma vijijini

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Serikali imesema itazitoza kampuni za simu zilizoshindwa kufikisha huduma ya mawasiliano kijijini ifikapo Julai Mosi mwaka huu kwa kushindwa kufikisha huduma vijijini kama walivyokubaliana na serikali, kampuni hizo ni Vodacom, TTCL, Tigo na Airtel,
hayo yalisemwa na waziri wa wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Makame Mbarawa wakati akizungumza na watumishi na wadau wa sekta hiyo Iringa
na ameikumbusha kampuni ya simu ya Halotel kukamilisha mkataba wake wa kufikisha huduma ya mawasiliano ya mtandao bure kwenye shule za vijijini zilizo na umeme na vituo vya huduma za Afya
 
Hiii nchi basi tuu, au mikataba yao na TCRA akati wanaomba vibali kuna kipengele cha usipofika kijijini unafutiwa kibali?
 
Hahaahahahhahahah hii nchi nawambieni comedy zimezidi. Ina maana mheshimiwa hajui hata theory ndogo tuu za uchumi kama demand and supply au capital management strategies? Kwamba "always capital flows from the area of low cost of production". Humo kuna vigezo vingi sana vya kuzingatia kabla ya kufanya investment yoyote. Kama market availability na accessibility.

Hiii nchi basi tuu, au mikataba yao na TCRA akati wanaomba vibali kuna kipengele cha usipofika kijijini unafutiwa kibali?
Mkataba wao umeusoma kwani... Kama Waliahidi kufikisha Huduma hizo kijijini Hayo mambo Yako ya Demand na Supply unayajua kwenye Vitabu vyako....

Watu hata Kwenu nahisi huwa hamjui kama mnawazazi na ndugu Vijijini
 
Mkuu swali langu hapo chini umeliona lakini? Unapaswa unijibu tuu kwamba kuna mkataba au makubaliano yanayosema hivyo.

Kuhusu kijijini, me ni mzaliwa wa huko huko na bado nipo huko na mtandao upo,huku tuna airtel 3G na Tigo3G. Ndio maana unaona natoa mawazo yangu hapa Jf
 
Mkuu mimi pia niko huku kijijini, japo naperuzi JF lakini mawasiliano kiujumla ni magumu sana!
Hapa nipo juu ya mti. Imagine huwa napanda mara ngapi kwa siku na risk za kuanguka n.k
Kama makablasha ya mkata waliahidi kufikisha huduma vijiji, aisee inabidi watekeleze make si kwa taabu hizi kwa sie tuliopendezwa kukaa kijijini!
 
Kama kilometa tano hivi kutoka wilaya ya ruangwa mkoani Lindi maarufu kwa WAZIRI mkuu wa hawamu ya tano kijiji kimoja kinaitwa Chunyu niliwahi kwenda huko mwezi may mwaka huu airtel tigo vodacom inasumbua kidogo halotel inajitahidi lakini mitandao mingine mpaka uvizie yani utafute kama vile unaseti dishi la TV ikikamata hapo hapo ndiyo unatulia ukitingishika tu network inahama siyo huko tu vijiji vingi vya Ruangwa network ni sheeda
 
Vipo vijiji kupiga simu mpaka upande juu ya mti au kichuguu au uende umbali mrefu kutafuta netwek.Mfano Moshi vijijini chini kusini kuelekea bwawa la Nyumba ya Mungu,Wakijenga Minara kijiji cha Mikocheni,Msitu wa Tembo au Magadini inaweza kusaidia eneo hili.
 
Back
Top Bottom