Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani anena mazito kwa Rais Magufuli

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
250
408
Mhe Rais, Mhe Mwenyekiti wa Chama chetu.. nikushukuru sana sana kwa niaba ya Wanawake wote walikuwepo hapa.. lakini na Wanawake Watanzania kwa kuonyesha imani yako kwetu.”*

“Mhe Rais au Mhe Mwenyekiti. ulisema jana kwamba uliponiteua mara ya mwanzo, hukuwa na uhakika sana. Lakini miaka ilivyokwenda, ukaona huyu ndio Mama wa kwenda naye awamu ya pili. Lakini nataka nikwambie Mhe; Nguvu niliyoipata kufanya kazi na ukawa na imani ukaridhika nami niliipata kwa Wanawake hawa.. Wanawake wa chama cha Mapinduzi, lakini pia Wanawake wa Tanzania. Kubwa zaidi nguvu uliyotupa katika kutekeleza yale wanawake tuliyotarajia Elimu kwa watoto wetu, Afya nzuri kwetu sisi wenyewe wakina mama na watoto wetu kila mahali; Lakini pia kutushusha ndoo.”

“Kubwa zaidi Mheshimiwa, ni lile la kutuletea umeme mpaka manyumbani! Sasa Wanawake tuna wasaa mzuri sana wa kufanya mambo ya maendeleo kwa kuwa ugumu wa maisha umerahisishwa mambo yetu mengi. Mhe Rais huyu ameyapigania na tumeweza kutafanikisha kwa kiasi kikubwa.”

“Mheshimiwa Rais, nisiwe na maneno mengi; Kwa niaba ya Wanaweke wote wa Tanzania na Wanawake wa Chama cha Mapinduzi, tukuahidi kwa mara nyingine tutakuwa bega kwa bega na wewe tutafanya kazi bila kuchoka ili kuipaisha Tanzania yetu.”

“Mwisho kabisa Mheshimiwa Rais nikupongeze kwa yote yaliyotimia katika kipindi hiki na nikupongeze kwa kuchaguliwa kwa kauli moja kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Asante sana Mhe.”- Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Ikulu, CHAMWINO Makao Makuu.

IMG-20200713-WA0171.jpg
 
Si yale yale tuu ya kusifia,
Kuna lipi jipya hapa?
Lipi zito lilio nennwa?
Au kampeni ndio zimeanza?

Zaidi ya asilimia 60% ya nchi haina umeme.
Zaidi ya Asilimia 70% haina maji ya bomba na salama.
Maji yako Mijini tuuna baadhi ya Vijiji.

Unaepuka takwimu zenu wenyewe?
Siasa bana Kweli si Hasa
 
Roho yako ina sumu mbaya sana Chief
Wahi Hospital ukaangaliwe vzr
 
Hotuba safi toka kwa mama wa nguvu Mama Samia .
Upinzani hawana mama wa nguvu wamejaza visichana vi sister du vikina Halima Mdee
Vyama vya upinzani Vimekosa malezi ya akina mama wa nguvu kama Mama Samia ,CCM tuna mama wa nguvu
Watu wenye heshima hawawezi CDM ya sasa, si unaona Profs Baregu na Safari wamekimbia?
 
Rais anaweza kumfuta kazi makamo wa rais, au inabidi akomae nae tu mpaka muhula uishe? Nauliza tu.
 
Katika mapungufu yote yaliyopo CCM na utawala wake, kwa huyu mama ndio sehemu pekee hawakufanya makosa.
Huyu Mama ambae baada ya wafanyabiashara kule Tunduma kulalamika TRA wanawapiga kodi ndefu wakawa wamehamishia shughuli zao Zambia,yeye alivyoenda kule akawaambia msihangaike nao hao waliohamia Zambia waacheni wala hatuwahitaji.

Ccm ni wale wale tu,utofauti wengine hua hawajapata sehemu ya kuonyeshea true color yao.

Nadhani Juzi Jaffo ameonyesha hili ninalosema kwa vitendo kwa yule meneja wa TARURA kule Arusha.
 
Rais anaweza kumfuta kazi makamo wa rais, au inabidi akomae nae tu mpaka muhula uishe? Nauliza tu.
Anafutwa fresh kabisa bila shida yoyote ile,kwa waziri mkuu akifanya hivyo ndio kuna shughuli kidogo hapo.
 
Bawacha wakikutana wote hawawezi toa hotuba iliyoshiba kama hii!
Hotuba zilizoshiba bila unafiki ni hizi. Mwanamke jasiri kama huyu baada ya kutoweka wa kina Bibi Titi Mohammed umepata kumuona wapi zaidi?
Fungueni akili zenu mtafakari kwa makini ushujaa huu wa Halima sio hayo mapambio ya madebe matupu.

Hotuba safi toka kwa mama wa nguvu Mama Samia .
Upinzani hawana mama wa nguvu wamejaza visichana vi sister du vikina Halima Mdee
Vyama vya upinzani Vimekosa malezi ya akina mama wa nguvu kama Mama Samia ,CCM tuna mama wa nguvu

Mbona unaponda Sana?Hawa wote kabla ya 1992 si walikuwa CCM?Kwa hiyo ni zao Lao.Pia sote tu watanzania, ndugu mmoja.
 
Mhe Rais, Mhe Mwenyekiti wa Chama chetu.. nikushukuru sana sana kwa niaba ya Wanawake wote walikuwepo hapa.. lakini na Wanawake Watanzania kwa kuonyesha imani yako kwetu.”*

“Mhe Rais au Mhe Mwenyekiti. ulisema jana kwamba uliponiteua mara ya mwanzo, hukuwa na uhakika sana. Lakini miaka ilivyokwenda, ukaona huyu ndio Mama wa kwenda naye awamu ya pili. Lakini nataka nikwambie Mhe; Nguvu niliyoipata kufanya kazi na ukawa na imani ukaridhika nami niliipata kwa Wanawake hawa.. Wanawake wa chama cha Mapinduzi, lakini pia Wanawake wa Tanzania. Kubwa zaidi nguvu uliyotupa katika kutekeleza yale wanawake tuliyotarajia Elimu kwa watoto wetu, Afya nzuri kwetu sisi wenyewe wakina mama na watoto wetu kila mahali; Lakini pia kutushusha ndoo.”

“Kubwa zaidi Mheshimiwa, ni lile la kutuletea umeme mpaka manyumbani! Sasa Wanawake tuna wasaa mzuri sana wa kufanya mambo ya maendeleo kwa kuwa ugumu wa maisha umerahisishwa mambo yetu mengi. Mhe Rais huyu ameyapigania na tumeweza kutafanikisha kwa kiasi kikubwa.”

“Mheshimiwa Rais, nisiwe na maneno mengi; Kwa niaba ya Wanaweke wote wa Tanzania na Wanawake wa Chama cha Mapinduzi, tukuahidi kwa mara nyingine tutakuwa bega kwa bega na wewe tutafanya kazi bila kuchoka ili kuipaisha Tanzania yetu.”

“Mwisho kabisa Mheshimiwa Rais nikupongeze kwa yote yaliyotimia katika kipindi hiki na nikupongeze kwa kuchaguliwa kwa kauli moja kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Asante sana Mhe.”- Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Ikulu, CHAMWINO Makao Makuu.

View attachment 1505354
mzee Pombe kasema sisi wasukuma tunapendaga sana weupe c mnajua,sasa namchagua tena mama Samia Suluhu,huyu mama ni mweupe ni mzuri akiingia tu pale ofisini hatakama nina sitresi zinakwisha ninafanya kazi vizuri hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
 
Back
Top Bottom