Makame wa NEC Tz kuwa kama Kivuitu wa NEC ya Kenya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makame wa NEC Tz kuwa kama Kivuitu wa NEC ya Kenya?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kalunguine, Oct 10, 2010.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Dalili zinaonyesha ushindi mkubwa kwa Dr Slaa wa Chadema kuwa rais mpya wa Tanzania. Lakini kuna kiza kinene kama matokeo yatakayotangazwa yatafanana na maamuzi ya wananchi katika kura. Je Jaji Lewis Makame wa NEC ya Tanzania atageuka kuwa Kivuitu aliyeleta balaa Kenya kwa kukubali kutangaza matokeo ya wizi, ama Makame ataamua kujiuzuru kukataa kutangaza matokeo yaliyopikwa na CCM ili kulinda heshima yake na ya nchi yetu?
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Makame akileta za Kenya Damu ya watanzania itakayomwagika kwa kupigwa maeneo tofauti tofauti Tanzania ili kukubali matokeo itakuwa juu yake
   
 3. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Maluweluwe si unayaona lakini, mara Shimbo, halafu REDET na sasa Takwimu za NEC zinazotia mashaka, huyu Makame naona kama anaishia huko.
   
 4. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Makame atake asitake lazima atangaze matokeo kama atakavyoelekezwa na 'mwajiri' wake. Hapo ndipo tutajua umuhimu wa kuwa na tume huru ya uchaguzi. Hivi mnatarajia afanye vinginevyo?

  "It's not the people who vote that count. It's the people who count the votes." - Josef Stalin.

  Na "wanaohesabu" na kutangaza matokeo tukumbuke ni NEC (inayomilikiwa na walio madarakani). Hivyo tujiandae kuhesabu maumivu! Ni ukweli ingawa unauma!
   
Loading...