RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Serikali imesisitiza kuwa haina mpango wa kusitisha ubomoaji wa nyumba za watu wanaoishi katika maeneo hatarishi, lakini itatekeleza utaratibu huo kwa kufuata misingi ya kibinadamu.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alipotembelea maeneo ya mabondeni kujionea hali halisi na changamoto zinazokumba zoezi hilo.
“Kila utaratibu lazima ukumbwe na changamoto na sisi tumezibainisha na kuzifanyia kazi, ni kweli wapo waliobomolewa lakini walipewa hati na vibali vya ujenzi vya serikali, ukweli ni kwamba kati ya makazi 774 yaliyokwishabomolewa ni makazi 20 tu ndiyo yenye hati hizo,” alisema January.
Hata hivyo, alisema serikali imebaini kuwa wananchi wengi ambao nyumba zao zimebomolewa, takribani asilimia 70 ni wapangaji na wenye nyumba wapo ambao walishafidiwa maeneo hayo na kuondoka, lakini baadaye wakarejea.
Amesema katika ziara yake hiyo, kuna maeneo ya aina tatu ambayo ni yaliyokwishabomolewa, yaliyowekwa alama ya X lakini hayajabomolewa na yaliyo katika mazingira hatarishi, lakini hayajawekewa alama.
Alisema katika eneo la waliowekewa alama kabla ya kubomolewa, aligundua wananchi wengi wako katika taharuki, ingawa walikiri na kuonesha kufahamu kuwa mazingira wanayoishi ni hatarishi.