Makamba akiri: Kuna wengi wana mashati ya kijani lakini moyoni sio hivyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba akiri: Kuna wengi wana mashati ya kijani lakini moyoni sio hivyo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 18, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TUMEKUWA TUKISEMA KUWA WENGI WA WANAOVAA MAVAZI YA CCM NI KWA HOFU YA KUPOTEZA KITU FULANI LAKINI KWENYE SANDUKU LA KURA WAO NAO SIO RAHISI WAISUTE DHAMIRI YAO JUU NI NANI ANAFAA KUWA KIONGOZI ANAYEWEZA KUTHIBITI UFISADI.
  Makamba amenukuliwa na mwananchi na hii ni sehemu ya alichokisema kwa kukubali kuwa hata walio na mashati ya kijani bado kuna ambao mioyoni sio.

  "Najua wapo hapa baadhi yetu wana mashati ya kijani lakini moyoni sio wenzetu, naowaomba kuanzia leo tushirikiane... ," alisema Makamba. Source Mwananchi Oct 18,

  NINASHUKURU KUWA WOTE TUNAONA UKWELI. KATIKA MIKUTANO YA CCM NUSU AU ZAIDI HAWATAIPIGIA KURA CCM. NINAMFAHAMU NDUGU YANGU MMOJA YUKO KWENYE KILA KAMPENI KWA SABABU ZAKE LAKINI KATI YA WANAOCHUKIA CCM YEYE NI NAMBARI WANI NA HUWA ANATUAMBIA WAZI. CHA AJABU HATA ALITAFUTA KUGOMBEA KWA CHAMA HICHO AKIWA AKIKICHUKIA HIVYO HIVYO. WAKO WENGI WA AINA HIZO ZA MASLAHI TU.

  NA SIO KWAMBA AKILI ZA KAWAIDA HAZIWAAMBII CHAMA KIMEFIKIA UKINGONI KWA KUWA HAKINA TENA CHOCHOTE KINACHOJULIKANA KUWA NDIO MSIMAMO WA CHAMA. Msimamo usioyumba wa CCM ni nini? Utaifa? Rushwa? Kupinga Ukabila? Ni kuchukia umaskini? Ni kupigania haki za wazawa? Ni kutetea wanyonge, machinga? Ni nini?
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mwaka huu kazi ipo. Ccm wamebanwa sana.
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Na bado,picha kamili 31 Oct 2010!
   
 4. X

  XWASSAU New Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Mtanzania wa leo si wa kudanganywa na mavazi ya magawo. Wanajua kuwa thamani ya kura zao si sawa na nguo za kijani. Japo wanavaa lakini si kuwa wamenunulika bali hwataki bughudhiwa. Kama mkubwa Makamba anafikiri nguo ndo ishara ya kura walizonazo basi atashangaa jua kuzama mchana. Bonde la mto Ruvu mjihadhari na ahadi mlizopewa kuwa wawekezaji wanakuja kulima mboga, kama hamjui yaliyowapata wenzenu wa Loliondo na wananchi wa maeneo ya machimbo mbalimbali ya madini basi wakaribisheni hao wawekezaji. Miaka 50 hatuwezi kulima mboga za majani hii ni aibu"
   
 5. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,912
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Yaani kuna watu wameweka mbele uchama kuliko utaifa. Tutafika kweli?
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hahahahaha,nakumbuka pale nilipo kua nimevaa "shati" langu lenye kijani na njano iliyo fifia,nilipokua natembea maeneo ya mikocheni alipita mzee na mkoko wake akanionesha kidole na kunipungia mkono,.....mdogo wangu akaniuliza "ana kufahamu" nikamjibu sijui......duh nilistuka baada ya kuvua shirt kumbe alidhani fisadi mwenzake hahahaha

  Natafuta wa kumpa shirt hii ingawa ni nzuri mno
   
 7. LOGARITHM

  LOGARITHM JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Makamba au sijui Makambo vile...si tu kuwa utalijua jiji mwaka huu, bali utaijua Tanzania na kizazi cha leo.

  Chagua DR. SLAA , chagua CHADEMA.
   
Loading...