Kwanza kabisa nitangulize shukurani zangu za dhati kwa wanaCHASO tawi la SAUTI-Mwanza, hawa makamanda kazi waliyoifanya ni kubwa mno, wamekiimarisha Chama kuanzia ngazi ya msingi mpaka uongozi wa juu. MASIKITIKO YANGU ni kwa makamanda wenzangu hapa UDSM mlimani, uongozi wetu jamani tunawaomba muungane kama viongozi wetu kitaifa wanavyofanya kazi kwa bidii. Makamanda tuungane pamoja kuijenga Chaso imara, kuwasajili wanaCHASO wapya na pia tujipanga kuanzia ngazi zote kama kawaida yetu, Ndg zangu nimeileta kwenu makamanda mkiwa mashahidi na kuona Jinsi gani nchi yetu inavyoenda kubaya katika misingi ya Elimu, uchumi na uongozi kwa ujumla. Sisi kama wanachuo embu tuifufue CHASO kama msingi wetu wa kutoa dira, Embu angalieni mfumo wetu wa elimu, Leo hii huwezi tofautisha mwanachuo na mtoto aliyeishia form4. Leo Hii Big-result now inakuwa na kuvuruga elimu na siyo kuandaa mazingira ya mwanafunzi kufaulu, je hii nchi wapi tunaenda?