Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema ushindi mkubwa wa CCM katika maeneo mbalimbali ni ushahidi wa wananchi kuridhishwa na utekelezaji mzuri wa ilani ya chama hicho, pamoja na miradi iliyotekelezwa na serikali yao.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wilayani Kilombero, mkoani Morogoro, Makalla alisema wananchi wameamua kwa hiari yao kuikabidhi CCM ushindi kwa sababu wanaona matokeo ya maendeleo katika maeneo yao, akisisitiza kuwa:
"Wamekipa ushindi Chama cha Mapinduzi kwa sababu wameridhika na utekelezaji mzuri wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM, wameridhika na miradi mbalimbali iliyofanywa katika maeneo yao nakuthibitisha hicho ndio maana wametuchagua tena kwa kura nyingi"
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima amesema tayari mashine za kudhibiti mafuriko zimeshanunuliwa kwa ajili ya kudhibiti tatizo la mafuriko katika Wilaya ya Kilombero.