Makalla aukataa uteuzi Simba, asema ni batili

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,363
Reaction score
18,652
Mkuu wa Mkoa wa Arusha na mwanachama nguli wa Klabu ya Simba, Amos Makalla, amepinga vikali taarifa za uteuzi wake kuwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Klabu ya Simba SC, akitangaza kuwa mchakato huo ni batili.

Soma: Magori: Kikao cha Bunju ni batili, haukuwa Mkutano Mkuu rasmi wa Simba

Kupitia ujumbe wake, Makalla ameweka wazi kuwa akiwa mwanachama anayeijua vyema Katiba ya Simba na taratibu zote za upatikanaji wa wajumbe wa baraza hilo, uteuzi uliofanywa umekiuka sheria na miongozo ya klabu.

Soma kuhusu Try Again arejeshwa Simba, aunda Baraza jipya la Wadhamini lililopitishwa na Wanachama Bunju

Kauli ya Amos Makalla: "Nimeona hii habari ya uteuzi kuwa mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Simba. Mimi ni mwanachama wa club ya Simba nafahamu vyema Katiba ya Simba na mchakato wa kuwapata wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa club ya Simba."

"Uteuzi huu ni batili, kwa sababu Katiba ya Simba haikufuatwa na mimi binafsi sikushirikishwa."
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜„
 
Sasa hii ndio Simba ninayoijua mimi. Simba ya migogoro.
Migogoro wanaitengeneza ili kutafuta visingizio watakapofungwa kwenye ngao ya jamii, au la wanataka mechi isiwepo kabisa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…