Makalio na mapaja makubwa ni bora kwa afya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makalio na mapaja makubwa ni bora kwa afya

Discussion in 'JF Doctor' started by M-bongotz, Jan 13, 2010.

 1. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Wadau katika pekua pekua zangu nimekutana na hii.....eti..

  Makalio na Mapaja Makubwa ni Bora Kwa Afya

  [​IMG]
  Wednesday, January 13, 2010 4:44 AM
  Wanawake wenye makalio makubwa na mapaja makubwa kama vile Beyonce na Jeniffer Lopez wana uwezekano mdogo sana wa kupata magonjwa ya moyo na kisukari kulinganisha na wanawake wenye makalio madogo, matokeo ya utafiti wa wanasayansi nchini Uingereza umeonyesha. Wanasayansi wa nchini Uingereza waliofanya utafiti wao katika chuo kikuu cha Oxford University wamegundua kuwa makalio makubwa yana faida kubwa zaidi kiafya kuliko matumbo makubwa (vitambi).

  Utafiti umeonyesha kuwa makalio na mapaja makubwa huhifadhi mafuta ambayo husaidia mwili kujilinda na magonjwa ya kisukari na magonjwa ya moyo.

  "Mafuta ya kwenye makalio na mapaja ni bora kwa afya lakini mafuta mengi ya kwenye tumbo si mazuri kiafya", alisema Dr Konstantinos Manolopoulos, mmoja wa watafiti watatu walioshiriki kwenye utafiti huo ambao matokeo yake yalichapishwa kwenye jarida la International Journal of Obesity.

  Watafiti hao walisema kwamba mafuta ya kwenye tumbo hutoa tindikali nyingi za mafuta zenye madhara kwa mwili wakati mafuta ya kwenye makalio na mapaja huzuia tindikali za mafuta zenye madhara kuingia kwenye misuli na maini na hivyo kuuepusha mwili na magonjwa ya kisukari na magonjwa ya moyo.

  Ingawa mafuta ya kwenye makalio na mapaja huyeyuka taratibu sana lakini mafuta hayo hutoa homoni zenye faida zijulikanazo kama adiponectin ambazo huilinda mishipa ya damu na kusimamia kiwango cha sukari mwilini.

  Wanasayansi hao walisema kuwa wanaendelea na utafiti ili kutengeneza dawa za kuufanya mwili uhifadhi mafuta yake kwenye makalio na mapaja ili kupunguza matatizo ya kiafya yanayosababishwa mafuta kujazana kwenye tumbo.

  Utafiti huo ulimalizia kwa kusema kuwa wanawake wenye mapaja au makalio madogo sana wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata matatizo kadhaa ya kiafya kama vile kisukari na magonjwa ya moyo.

  SOURCE:http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3917698&&Cat=7
   
 2. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Imekaaje hii..karibuni tuchangie..
   
 3. GP

  GP JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mhhhh
  hii itasababisha matatizo makubwa sana.
  kutatokea MIJIKALIO na MIJITAKO ya ajabu sana.
  maana juzkati nilkua pale mwenge jioni hivi nangoja bus, ilinilazimu kukaa zaidi ya lisaa limoja nikithaminisha jinsi wachina wanavyoharibu dada zetu kwa madawa yao ya ajabu, yani we acha tu. siku hizi kina dada makalio ni fasheni au????????
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kikombe hichi naomba KINIPITE!.....
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mchina atatajirika sasa ingawa hao watakaovimbisha makalio yao na MCHINA ndo watapata madhara zaidi lkn hawatajali hiloo. Mh! na hao Models sasa watakimbilia CHINA akina Naomi Campbell?. Ghafla ikatokea preference ya wanaume wa kiafrika ikabadilika na kuanza kuthamini vimodo hawa wenye makalio wataenda clinic kuyatoa au?
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
   
 7. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  We mziwanda wewe hiyo habari nimeiquote tu toka kwenye chanzo kingine, si mimi bali ni wao ndio walioandika Beyonce au Jeniffer Lopez, kwani hujaona source mwisho wa hiyo habari.
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  sio kila **** ni la mchina kaka!! dada zetu wamebarikiwa atii!! mengi tu ni yaukweli kabisa.......lol!!
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  sos nimeiona ila na wewe inabidi habari uicustomize iendane na mazingira halisi. ukija bongo, JLO na BEYONCE ni vimodo tu
   
 10. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  kweli dongo unapenda sana haya mambo.
  kuanzia avator yako hadi post zako.
  weee ni kiboko ya hii kitu[​IMG]
   
 11. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Sikutaka kuicustomize kwani nimgepoteza maana ya ku-quote
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaaaa eeeh baba niepushe na kikombe hiki
   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yani sijui miaka ijayo watanzania watakuwa kwenye wakati mgumu wakujua vifaa feki na org na kumjua mwanamke feki na org mungu saidia
   
Loading...