MAKALA: Kwanini wanaume husaliti penzi kila wakati?

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Leo tunazungumzia ni kwanini wanaume wengi hupenda kutoka nje ya ndoa zao ama kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.

Haimananishi kuwa mwanaume anapotoka nje ya mwenzi wake amemchoka ama hamtaki, kinachotokea ni kwamba mwanaume huvutwa na hali halisi ya maumbile ya mwanamke na kila wakati hupenda kutafuta ladha fulani.

Kujua kuwa mwanaume huyo anamheshimu mpenzi wake wa kudumu, atakuwa anafanya mapenzi hayo ya wizi kwa siri ili mpenzi wake ama mkewe asitambuwe kuwe anaibiwa.

Mara nyingi wanawake huwa hawapendi kuwaona wenzi wao wakiwa na uhusiano wa mapenzi na mwanamke mwingine zaidi yake hivyo huwa na wivu mkubwa juu ya mpenziwake kufikia hatua ya kuwekeana uhasama na mwanamke atakayemgundua kuwa anamwibia penzi lake.

Ugomvi mwingi wa wanawake unakuja pale ambapo wanajikuta wakishea mwanaume mmoja na kwa wkati mmoja huku kila mmoja akiwa na tumaini kuwa yuko pekeyake na mwanaume huyo kumtimizia kila mmoja haki yake kwa muda wake.

Wanawake hao watakapogunguana, ajabu wanawekeana uhasama wao kwa wao bila kujua kuwa kati yao hakuna mwenye kosa kwani kila mmoja kwatakwa kwa muda wake na wakumlaumu ni yule mwanaume ndiye wangepaswa kukkaba awaeleze kinagaubaga.

Haimaanishi kwamba wanume ni malaya sana kuliko wanawake ndio maana hawatosheki matamanio yao, lahasha! hapa tunayazungumzia maumbile ya mwanaume kutokana na kuvutika kihisia kwa mwanamke yeyote amwonaye kuwa na mvuto kwake.

Wakati mwingine wanawake tumekuwa kivutio kwa wanaume na kuwaweka katika wakati mgumu huku tukielewa wazi kuwa tunawatega. Pamoja na kuwa tunakwenda na wakati, tunapaswa kujua kuwa mwanamke hata avae juba, mwanaume akishamtamani lazima akidhi haja ya matamanio yake hata kama hatafanikiwa kwa mwanamke huyo, basi atatafuta mwanamke anayeendana na huyo.

Hayo ndiyo maumbile ya mwanaume hivyo kwa mwanamke mwenye wivu unaweza ukajidhani labda humvutii mpenzi wako ama hupendezu kumbe wewe ni mzuri na unawavutia wanaume wengi kwani hakuna mwanake asiyekuwa na mvuto mbele ya mwanaume.

Ili kujua kuwa mwanaume anakupenda ila hufanya kosa kutokana na maumbile yake, ni pale utakapomfumania akikusaliti, mwingine hukosa raha ama akajikuta akilia kujutia alichokifanya huku akiwa na hofu ya kuachwa.

Mwanaume mwingine huwa anakosa cha kuongea na kupata kigugumizi cha ghafla ama kujikuta akikudanganya juu ya tukio hilo kuwa hakutegemea kama ingetokea, “Hakujua kama angefanya”, kwa wanaume wengine hukujia juu ili kukupunguza jazba ama kukutisha ili usimuulize chochote na kisha baadae hukuomba msamaha. hizi zote ni baadhi ya tabia na maumbile ya wanaume.

Wapo ambao wanawatetea wanawake wanaofumaniwa nao kwa ajili ya kuwalinda isi wasidhuriwe na mwanamke muhusika kwani yawezekana lolote likatokea kati yao kisha mwanaume yule akaja kukuomba radhi na kukusihi kuwa hatorudia kosa hiyo imetokea kwa bahati mbaya akashindwa kujizuia.

Jinsi ya kujikinga na na kujaribu kumfanya mpenzi wako asiwe na tamaa, mwache awe huru na mjengee mazingira ya kuona wivu na kuhisi kuwa anaibiwa. kwa kufanya hiyo unaweza ukamweka mwanaume wako katika mtihani na kumpa kazi kubwa ya kukufuatilia hatua hadi hatua na kujikuta akikosa muda wa kuwatizama wanawake wengine hivyo unakuwa umemwondolea tabia ya kuwatamani wanawake ovyo na kumpa kazi ya kukuchunga.

Haimaanishi kuwa mkawafanyae waume zenu hivyo, kwa kuwakomoa, jaribuni kuwafanyia ili kutengeneza penzi lenu. wapo ambao hawajali ukimwacha huru anashukuru na anakuwa naye anakuacha huru japo atakuwa anaumia kuwa huenda anaibiwa, atauficha wivu wake juu yako.

Hakuna mwanaume anayependa kuona kuwa anashea mwanamke na mwanaume mwenzake, huwa inawaweka katika wakati mgumu na niadhabu kubwa inayowaumiza japo wanakuwa jasiri tofauti na wanawake wanaoishia kulia na kujikondesha.

Hii ni tabia ya baadhi ya wanaume wengi kwani wivu wao upo ndani na unawaumiza ndani kwa ndani lakini hawapendi kuwaonyesha wanawake kuwa wanawivu juu yao.

Mwanaume huwa atakuuliza tu kuwa yule ni nani na kwanini umesimama naye ama umekaa naye sehemu ya stare au faragha kama hiyo na hapo hapo atataka mchezo ili kuhakikisha kuwa hakuna aliyepita kwenye njia yake.

Nataka nikwambie jambo moja wewe mwanake mwenzangu ambaye unadhani kuwa labda mpenzio anakuona humzuri ndio maana anatoka nje na kukuacha ndani peke yako.

Kwanza usisuburikusifiwa kuwa wewe ni mzuri, cheo hicho jipe mwenyewe na anayekuona kuwa wewe ni mbaya usimkataze kufikiri hovyo kwani huo ni matazamo wa akili yake unavyodhani lakini amini wewe umzuri kuliko mtu mwingine yeyote.

Pia usipende kumsema mwanamke mwenzio kuwa si mzuri, Mungu hajaumba binadamu vibaya ila tabia ndio zinatofautiana kutokana na maumbile ya nafsi ya mtu mwenyewe upeo wa akili zetu.

Mwanaume wako anapotoka nje na ukajua, usimwambie chochote zaidi ya kumsifia kuwa anachombo kipaya na kizuri kisha mpe hongera na atakapo mambo fulani mpe, utakapomfanyia hivyo utamnyima raha kwa kujutia alichokifanya na kuwaza kwanini amekusaliti.

Japo kuwa ni maumbikle yamempelekea kufanya hivyo, atajilaumu na wakati mwingine atakuwa anataka kukufanyia jambio ili usahau ama umsamehe zaidi kosa lake la kusaliti penzi. Wakati mwingine wanawake wanapowafumania waume zao huanza kuropoka na kuwatukana, mmm! hatuendi hivyo dada yangu, unapomfumania mwanaume wako msifie kwa urijali wake na kisha nyamaza kimya bila kumuuliza chochote.

Kama ilivyo kawaida ukimya ni adhabu kwa wapendanao, unaponyamaza atataka kujua kuwa unafikiria nini kichwani kwako, atakosa raha kwa kujua kuwa huenda ukalipiza kisasi, atawaza mengi juu ya ukimya wako na ukamfanyia hivyo kwa wiki moja, ukaenda kumpima uzito atakuwa amepungua.

Yapo mambo mengine yanayopelekea mwanaume kusaliti penzi lake
kutokana na jinsi mpenzi wake anavyojiweka tofauti na kuwa maumbile ya mwanaume ni yamatamanio aonapo maumbile ya mwanamke.

Uchafu wa mwanamke nao unasababisha mwanaume kukimbilia anapoona kuwa panausafi na pengine kujikita huko kabisa japo wanadai kuwa gari huwa lazima ipate spea tairi, waweza ukajikuta kuwa, mazingira uliyonayo yanakufanya wewe ndiye spea kuliko spea yenyewe.

Nataka kuwashauri wanawake wenzangu kuwa mwanamke mazingira.
Kujipakaa mafuta usoni ukang'aa lakini kule Ikulu iliyokufanya wewe ukaitwa binti na kuonekana mrembo huifanyii usafi kiasi cha kumkera kila anayeingia, jua utakuwa mtanashati wa uso na mavazi tu lakini kwimgineko mh! Hapafai.

Tambua kuwa hiyo Ikulu yako ndiyo inawasababisha hao wanaume mpaka wanapigana, yote ni kwasababu tu inamvuto na ndio maana waweza kumuona mwanaume anamng’ang’ania mwanamke ambaye hawaendani, eidha mwanaume ni mzuri sana kuliko mwanamke lakini hiyo si tija cha msingi ni umaridadi wa Ikulu.

Wahenga walisema si vyote ving'aavyo ni dhahabu ati, pia Uzuri wa mkakasi ndani kipande chamti na mimi nakwambia kuwa, kaa na marashi nawe unukie japo hujajipulizia lakini ukaapo na wenye marashi nawe waweza onekana ni miongoni wao kumbe la.

Napenda wanawake tupunguze wivu na kwani unasababisha kujengeana majungi na wakati mwingine kudhiriana hata kwa kuuwana kisa ni wanaume ambao hata ufanye nini hakuna mwanaume wa pekeyako. Kasema hadija kopa kuwa Kama unaweza mtie kamba mumeo lakini ukitahamaki kachimba chini ninaye.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Mimi nakataa kuwa eti 'wanaume wengi hupenda kutoka nje ya ndoa zao ama kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.'

Naamini hiyo ni dhana potofu hadi pale nitakapoona takwimu za kuweza kuubadili mtazamo wangu.

Lakini mpaka wakati huo, suala la kutoka nje ya ndoa au uhusiano ni ngoma droo!
 
Kwa wende ndoa, wanawake wengi hawawatoshelezi waume zao. Mume akitaka mara anyimwe, mara apangiwe ratiba bila sababu za msingi. Basi ilimradi ni shiiiiiida!
 
kwani nyie wanawake hamtoki??? nyie mkishikwa mnalalamika lakini kuumiza mwanaume mnaurah! na bado malipo ni hapa hapa dunian tuu wanafiki nyoe.
 
Back
Top Bottom