Makala: Kupaa na Kutunguliwa kwa Azimio la Arusha, Ujio wa Magufuli na tumaini jipya...

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
* KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA, UJIO WA MAGUFULI NA TUMAINI JIPYA...

Rais Magufuli ana vita kubwa. Ni vita vya kulitoa Taifa letu katika hali ya unyonge na kulitia katika hali ya nguvu. Vita vya kuwafanya watanzania watoke katika hali ya dhiki na kuwa katika hali ya neema. Vita vya kupambana na wezi, wabadhirifu na majambazi wa mali za umma, hasa watumishi wasio waaminifu na wakuu wa mashirika ya umma wanaojilimbikizia mali kana kwamba mwisho wa dunia ni kesho

Magufuli ana vita vya kupambana na mafisadi walioota mapembe ya kibebari. Vita vya kupambana na wafanyabiasha waliozoea kukwepa kodi kwa miaka mingi. Vita vya kupambana na viongozi watakaojificha kwa nyuma huku wakipanga mikakati ya kumwangusha katika kutekeleza majukumu yake ya kutumikia wananchi. Vita vya kupambana na makabaila. Vita vya unyonyaji unaofanywa kwa wakulima na kubwa zaidi ni vita vya kupambana na umasikini uliokithiri, ambao kwa kiasi kikubwa umechochewa na mfumo ulioasisiwa tokea 1986

Rais Magufuli, baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka madarakani, wananchi tuliaminishwa katika "Fedha" na kuona kwamba maendeleo huletwa na fedha. Huu sio upotoshaji tu bali ni njia iliyotumika kukomaza ubebari kama sio ubeberu. Ndio mana leo hii viongozi wengi wa serikali wanajilimbikizia mali ovyo ovyo, na ndio mana tunashuhudia wakuu wa baadhi ya mashirika ya umma wanapokea zaidi ya millioni 36 mshahara. Ambao rafiki yangu Mtatiro kapiga mahesabu na kukuta mshahara huo wa millioni 36 kwa mkuu wa taasisi ni mshahara wa walimu 60. Au mshahara wa miezi 72 kwa mwalimu moja

Mheshimiwa Rais, naomba nikumbushe kuwa Azimio la Arusha linatuambia kwamba maendeleo ya nchi huletwa na watu, na hayaletwi na fedha. Fedha ni matokeo, siyo misingi wa maendeleo. Ili tuendelee Baba wa Taifa alisema tunahitaji vitu vinne (i) Watu (ii) Ardhi (iii) Siasa safi na (iv) Uongozi bora. Na malengo yetu tutayafikia kwa kufata marshati ya maendeleo, kama muongozo wa Azimio la Arusha linavyosema. Juhudi, maarifa, uchapakazi, kutoendekeza majungu&fitina, upendo na kuwajibika

Mh. Rais, Azimio la Arusha bila sababu za msingi lilidunguliwa ili tu iwape fursa viongozi na familia zao waliokuwa na uchu wa kujitajirisha kwa njia zozote zile. Ndio maana leo viongozi wengi kama sio wote wamekimbia miiko ya uongozi, na kutupilia mbali misingi ya Azimio la Arusha.

Leo hii viongozi wengi ni wafanyabiashara na sio wakulima au wafanyakazi. Leo hii viongozi wengi wana hisa katika makampuni mbalimbali. Leo hii viongozi wengi wanashirikiana na makabaila au mabebari kupiga dili. Leo hii viongozi wengi wana mishahara miwili au zaidi. Leo hii viongozi wengi wanafurahia na kuchekelea posho. Leo hii nyumba nyingi za kupangisha zinamilikiwa na viongozi. Shule nyingi binafsi na za ada kubwa zinamilikiwa na viongozi. Ndio mana Mh. Rais tunasema kwamba huu ndio muda mwafaka wa kurejesha misingi ya Azimio la Arusha. Hatuna muda mwingine zaidi ya sasa!.

Rais, tambua ya kwamba una kundi kubwa nyuma yako, na wananchi wengi tunakuunga mkono katika harakati zako za kutumbua majibu. Watu wanaoogopa mapinduzi ya leo unayoyafanya ni wanyonyaji; na wote wanaoogopa mabadiliko ni wanyonyaji tu; watu walioshiba ndio wanaoogopa mabadiliko, kwa sababu mabadiliko hayo yanawapa mashaka ya majipu yao.

Lakini, ni lazima watambue kwamba mnyonge lazima atake mapinduzi, mnyonge hawezi kutaka mambo yaendelee hivi hivi huku ananyonywa. Kamwe mnyonge hawezi kutaka hali hiyo. Wanaoshikilia hilo ni wale walioshiba si wanyonge (1973, Ujamaa ni Imani; Moyo kabla ya Silaha)... Ndio maana Mh. Rais wanyonge wote wanafuraishwa na kukuunga mkono kwa hatua unazochukua za kutumbua majibu!..

Mchambuzi Huru: Peter Kasera.... (BA Sociology.... MA Development Management. ... Phd (on progress)....
 
Back
Top Bottom