Habar Zenu
Mwenzunu nimejikuta kwenye wimbi la mawazo Baada ya kuelemewa na majukum. Baada ya Kupata kibarua nimejikuta napokea simu nyingi kuhusu Matatizo ya kifamilia
Nimejitahid sana kutatua Matatizo Kwa kadri ya uwezo wangu lakini mambo yanazidi kuwa magumu.
Ukiachana na kuhudumia familia Yangu lakini shida za Ndugu zimekuwa haziishi
Zinapokaribia tarehe za mwisho wa mwezi najikuta sina raha Kabisa maana napigiwa simu nyingi za shida na kuombwa pesa tu
Naombeni mbinu ya kukabiliana na changamoto hizi