Wana JF ninaomba mnijuze majukumu ya mh.Lukuvi,mara nyingi namwona ni mtu wa kuomba mwongozo,kutoa taarifa na kutetea viongozi wabovu serikalini, kwa mfano mwaka jana aliomba mwongozo kupinga ya hoja ya mh. Zitto Kabwe kufuatia maamuzi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi kumrejesha Jairo kazini na juzi amemtetea sana Mkulo kwa kutokuwepo katika kikao cha Bunge.
Je,wadhifa huu una tija kwa maendeleo ya nchi hii?