Majukumu ya JWTZ
JWTZ lilianzishwa tarehe 01 Septemba, 1964 likiwa na lengo la kulinda uhuru, na mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
JWTZ lina majukumu yafuatayo
:
- Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Kufanya mafunzo na mazoezi ili kujiweka tayari kivita wakati wote.
- Kufundisha umma shughuli za ulinzi wa Taifa.
- Kushirikiana na mamlaka za kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa.
- Kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
- Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji mali kupitia Jeshi la Kujenga Taifa.
- Kushiriki ulinzi wa amani kimataifa. source