Ni kweli uyasemayo, wengi hatuna uhuru wa kiuchumi kwa hiyo tunajitahidi angalau kujenga mazingira mazuri ya usimamizi wa fedha kwa kadiri baba wa familia anavyoona inafaa, wengi wetu wanaume ndio wamekuwa wasimamizi wa fedha na mwanamke anapohitaji fedha basi atapewa kadiri ya mahitaji yake au kilichopo.
Mimi binafsi sipendi kuombwa fedha na wife naye hapendi kuomba mara kwa mara fedha kwa ajili ya mahitaji ya nyumba, tunachokifanya ni kununua mahitaji ya msingi ya nyumbani kwa wingi yanayotunzika na kisha kuacha fedha mezani kwa ajili ya matumizi madogomadogo ya nyumbani.
Tuliwahi kujaribu kupanga bajeti ya mwezi mzima pamoja kisha nikamuachia fedha mke wangu, fedha zilikwisha baada ya wiki tu. Nikaachana na utaratibu huo