Majukumu ya Bunge ni kutunga Sheria na Kusimamia Serikali

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,670
Majukumu muhimu ya Bunge ni kuandaa, kutunga (kupitia, kurekebisha na kufuta) sheria pamoja na kusimamia utendaji wa Serikali. Katika demokrasia, Wabunge hutekeleza majukumu hayo kama wawakilishi wa watu.

Ili kutekeleza majukumu yake muhimu, chombo cha kutunga sheria, lazima kiwe taasisi mathubuti yenye madaraka na uwezo wa kuzuia maamuzi ya Mamlaka ya utendaji (Serikali) na kuhakikisha kwamba Mtendaji (Serikali) anafanya hivyo kwa uwazi na uwajibikaji. Kwa kufanya hivyo Bunge utekeleza wajibu wake kwa "usawa na uwajibikaji".

Bunge huru na lenye meno, huhitaji nyenzo mbalimbali za kufanyia kazi:
1) Rasilimali mali (majengo, miundo mbinu, mitandao, nk)
2) Rasilimali watu (wenye taaluma mbalimbali, ujuzi na uzoefu)
3) Asasi na utawala kusimamia na kuratibu shughuli za Bunge.

Je, bunge letu linajitosheleza kwa hayo, kiasi cha Wabunge na baadhi ya wananchi kutaka lioneshwe "live"!

Pia kuna masuala yafuatayo yanayowagusa wabunge moja kwa moja:
1) Uwakilishi bungeni uliotukuka.
2) Uwezo na kiwango cha Bunge kuisimamia Serikali.
3) Uwezo wa Bunge kutunga sheria.
4) Uwazi na upatikanaji wa taarifa za Bunge.
5) Uwajibikaji wa Bunge na Wabunge
6) Kiwango cha Bunge kujihusisha na Sera za Kimataifa.

Bunge letu linafikia kiwango gani katika hayo, ili suala la kuoneshwa "live" lipewe kipaumbele.
 
JF hakuna Mbunge mwanachama atusaidie kutupa tathmini ya ufanisi bunge la sasa, kabla ya kudai waonekane "live". Mada inakuwa mwiba kwao, au!
 
si kwa bunge hili la Tulia Akson Job Ndungai! Hili ni kinyume chake.
 
Majukumu muhimu ya Bunge ni kuandaa, kutunga (kupitia, kurekebisha na kufuta) sheria pamoja na kusimamia utendaji wa Serikali. Katika demokrasia, Wabunge hutekeleza majukumu hayo kama wawakilishi wa watu.

Ili kutekeleza majukumu yake muhimu, chombo cha kutunga sheria, lazima kiwe taasisi mathubuti yenye madaraka na uwezo wa kuzuia maamuzi ya Mamlaka ya utendaji (Serikali) na kuhakikisha kwamba Mtendaji (Serikali) anafanya hivyo kwa uwazi na uwajibikaji. Kwa kufanya hivyo Bunge utekeleza wajibu wake kwa "usawa na uwajibikaji".

Bunge huru na lenye meno, huhitaji nyenzo mbalimbali za kufanyia kazi:
1) Rasilimali mali (majengo, miundo mbinu, mitandao, nk)
2) Rasilimali watu (wenye taaluma mbalimbali, ujuzi na uzoefu)
3) Asasi na utawala kusimamia na kuratibu shughuli za Bunge.

Je, bunge letu linajitosheleza kwa hayo, kiasi cha Wabunge na baadhi ya wananchi kutaka lioneshwe "live"!

Pia kuna masuala yafuatayo yanayowagusa wabunge moja kwa moja:
1) Uwakilishi bungeni uliotukuka.
2) Uwezo na kiwango cha Bunge kuisimamia Serikali.
3) Uwezo wa Bunge kutunga sheria.
4) Uwazi na upatikanaji wa taarifa za Bunge.
5) Uwajibikaji wa Bunge na Wabunge
6) Kiwango cha Bunge kujihusisha na Sera za Kimataifa.

Bunge letu linafikia kiwango gani katika hayo, ili suala la kuoneshwa "live" lipewe kipaumbele.
Kama ni hivyo, wabadili sheria ili wagombea ubunge wawe wanasheria ili wakatunge sheria kama vile ukitaka kazi ya kutibu mgonjwa lazima uwe Daktari.
 
Hizo zote ni kazi za Bunge
. Kutunga sheria
. Kuisimamia serikali.
. Kuthibitisha (ratify) mikataba ya kimataifa.
. Kumwajibisha mkuu wa nchi na PM n.k

Bunge ndio chombo chenye uwakilishi wa watu, na watu ndio wanaoweka serikali madarakani na ikibidi kuiondoa pia.
 
Utaratibu wa utungaji sheria pale bungeni unaanzia wapi?
 
Back
Top Bottom