Majipu yataondoka na CCM

Majipu yataondoka na CCM

ccm ikifa nchi inaweza ikapiga hatua,

lakini kama ccm bado ipo hai,hata tuletewe malaika nchi hii itabaki palepale
 
WIKI iliyopita, Rais John Magufuli aliitisha mkutano wa ghafla kukutana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya mikoa na wilaya zote nchini, anaandika Ansbert Ngurumo.

Mwaliko huo ulikuwa wa ghafla na uliambatana na sharti moja kuu la viongozi hao kutofika Dar es Salaam wakiwa wamevaa sare za chama.

Gharama za safari zililipwa na Ikulu na makada hao waliondoka wakifurahia jinsi Ikulu ilivyowakarimu kwa chakula safi, kingi na cha kusaza!

Mkutano huo ulifanyika Ikulu na ilionekana wazi kuwa, waandaaji walikuwa ni maofisa wa Ikulu. Abdulrahmani Kinana, Katibu Mkuu na vijana wake wa makao makuu, hawakuwa na raha.

Walionekana wazi kuchoka na kusubiri mkutano huo uishe ili waendelee na shughuli zake nyingine.

Baada ya kufika katika ukumbi wa mkutano huo, hata itifaki za kawaida za mikutano ya ndani ya CCM zilikuwa hazieleweki, jambo lililomfanya Kinana kusimama mara kadhaa kurekebisha hapa na pale ili mambo yaende.

Kinana alikuwa na ujumbe mmoja kwa washiriki – kwamba mwezi Juni mwaka huu, Rais Magufuli atakabidhiwa chama kama mwenyekiti.

Kabla ya mkutano huo, nje ya ukumbi wa mikutano Ikulu na kwenye hoteli walikofikia makada, gumzo kuu lilikuwa ni kama CCM itakuwa salama chini ya Magufuli.

Wapo waliojidanganya kuwa Jakaya Kikwete, mwenyekiti wa sasa, hawezi kukabidhi chama mpaka 2017. Mashabiki hao wa Jakaya walisema Rais Magufuli aachwe aendelee na kazi ya kutumbua majipu serikalini, chama kibaki na Jakaya, ili kibaki salama.

Pale ukumbini, baada ya Kinana kutangaza kuwa Rais Magufuli atakabidhiwa chama mwezi Juni, kundi dogo la makada mashabiki wa Magufuli walishangilia, huku wakijishtukia wenyewe kwa wenyewe.

Walio wengi hawakuona sababau ya kushangilia kwa sababu kwanza ni utaratibu wa kawaida kufanya hivyo, na pili, kushangilia ni sawa na kusema wamechoka na uongozi wa Jakaya.

Baada ya mgongano ya kiitifaki, Rais Magufuli alipata nafasi ya kuwahutubia. Kwa kusudi la makala hii nitataja machache ya aliyozungumzia.

Kwanza, alisema amewaita viongozi hao kuwashukuru kwa kumpigania hadi akachaguliwa kuwa rais. Alikiri kuwa bila wao, asingekuwa hapo alipo. Pili, aliwaeleza kuwa amewaita kuwahakikishia kuwa nchi iko salama na chama kitakuwa salama.

Tatu, alisema amewaita kuwahakikishia wale wenye mashaka na kasi yake ya utumbuaji majipu, na walioanza kupinga hatua hizo waache kumkatisha tamaa. Akatumia muda mrefu kueleza baadhi ya hisia zinazoenezwa kuwa anakiuka haki za binadamu, kuwa mizigo bandarini imepungua, na kuwa atadhalilisha CCM.

Mpaka hapa kuna mambo mawili makuu ya kutazamwa kwa umakini. Kwanza, Rais Magufuli alifanya kampeini kwa kusisitiza, “Tanzania ya Magufuli” itafanya hili na lile. Alikuwa mwangalifu sana kutotanguliza CCM mbele ya umma uliokuwa umekata tamaa na CCM.

Hata baada ya kuapishwa, mara mbili ametofautiana na Kikwete katika vikao vya kamati kuu. Mara ya mwisho walitofautiana kuhusu suala la uchaguzi wa Meya wa Jiji la DSM.

Katika kikao hicho, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu walilalamika kuwa kuna mawaziri na watumishi wa serikali wanashabikia uchaguzi ufanyike na meya atoke Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi).

Kikwete aliunga mkono na kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya wote walio serikalini na wanashibikia jiji liende Ukawa. Kabla ya kuhitimisha ajenda hiyo, Rais Magufuli akaomba kuzungumza.

Katika mchango wake, akakiri kuwa wapo wanaounga mkono na yeye ni mmoja wao. Akasema kama ni kosa lilifanyika pale CCM iliporuhusu uasi ndani yake na kusababisha mkoa wa Dar es Salaam uwe na madiwani wengi wa Ukawa.

Akakumbusha kuwa hata yeye wakati wa kampeni alifika mahali akaacha kwenda kwenye vikao vya usiku vya kufanya tathmini ya kampeini kwa sababu ya fitina na uasi.

Akasisitiza kuwa kama CCM haitaacha majungu, yeye hatakuwa tayari kuitetea. Akahitimisha kwa kusema, ni vizuri “tuwaache Ukawa watutawale Dar es Salaam ili tuonje uchungu wa kutawaliwa kwa sababu ya uasi wetu”.

Baada ya mchango wa Magufuli, Jakaya Kikwete aliahirisha kikao kwenda kunywa chai. Mgongano huu wa Kikwete na Magufuli hauwezi kuiacha CCM ikawa salama.

Hii ni kwa sababu huwezi kusifia hatua anazochukua Magufuli bila kulaani uongozi wa Jakaya. Mpaka sasa Magufuli hajaanzisha jambo jipya serikalini, bali anachofanya ni kukosoa utendaji wa Rais Kikwete.

Kwa hiyo, tangazo kwamba Magufuli atakabidhiwa CCM mwezi Juni si tangazo la heri kwa CCM ya Kikwete. Ni tangazo la kutumbua majipu ndani ya CCM yakiwamo yale yaliyomwezesha Magufuli kuingia madarakani.

Hata kama Magufuli anatamba hadharani kuwa hakuna mfanyabiashara yeyote aliyemchangia hata senti moja, lakini CCM na vyombo vyake vilifanya madudu makubwa kumwezesha Magufuli “kushinda” urais.

Matajiri walichangia CCM iliyokuwa inamnadi yeye. Je, yuko tayari kufumua hata jipu hilo?

Jambo la pili ni ukweli kuwa majipu anayoyatumbua Magufuli si ya wapinzani bali watendaji wa serikali ya CCM. Kwa hiyo, majipu yanayotumbuliwa ni matawi lakini. Mashina ya majipu ni CCM.

Je, uking’oa shina mti utapona? Huu ndiyo wasiwasi unaoikumba CCM ikiwa mikononi mwa Magufuli. Kwa hiyo, wana CCM wanaoijua CCM wanajua kuwa CCM haitakuwa salama, ingawa yeye aliwahakikishia kuwa itakuwa salama.

Kwanini alilazimika kuwahakikishia usalama? Magufuli anaishi kwenye nadharia kuwa mafisadi ndani ya serikali na ndani ya chama, hawakutumwa na chama kufanya uchafu.

Magufuli anaishi katika njozi kuwa anaweza kutumbua majipu yaliyo katika sehemu nyeti – tena bila ganzi – halafu mgonjwa akabaki kuchekelea na kushangilia.

Wenye hekima na wazee wa chama wanajua majipu mengine yameumbwa ndani ya CCM, na ndiyo yanashikilia uhai wa CCM. Ukiyatumbua, umeitumbua CCM. Hata kwa hekima ipi, hayatumbuliki. Na yakitumbulika, yanaondoka na CCM.

Ufisadi wa mabilioni na mikataba feki ndiyo imeifikisha CCM na serikali yake hapa ilipo. Hata kwa kitendo cha Magufuli kuita makada wa CCM kwa kutumia fedha ya serikali wakati akidai kubana matumizi, tayari ametengeneza kipere kitakachogeuka jipu.

Uzoefu pale Ikulu na Lumumba – makao makuu ya CCM – ni kuwa mikutano ya namna hiyo hutumia mara tatu ya gharama halisi.

Hiyo ndiyo CCM atakayokabidhiwa Magufuli mwezi Juni. Magufuli hajui CCM. Kama angeijua, asingeikaribisha Ikulu kwa ajili tu ya kuihakikishia kuwa itakuwa salama yake.
\
\
boya kabisa!

Ni habari yenye lengo la kufitinisha! N mwaandishi anaonyesha wazi kufanya kazi hii maluumu kwa kutumwa na watu maalumu, na hasa ili kujenga hofu kwa mtumbuaji!

Kuna wanachama na baadhi ya viongozi waandamizi wanajiona wao ndio CCM na kwamba kuguswa wao ama ufisadi wao, ni kukigusa chama! CCM siyo mtu ama genge la watu hasa wahuni na wahujumu wa uchumi!

CCM kimepoteza wanachama wengi na hasa imani kwa wananchi kutokana na wahuni wachache wanaojiona wenyewe ndio Chama Cha Mapinduzi! Na imlikuwa ni vigumu sana kukinadi chama kwa jinis vile kilinuka katika uchaguzi uliopita! Wananchi walikichoka!

Ili kukiimarisha Chama, ni lazima haki itendeke na Haki hiyo ionekane inatendeka mbele ya jamii kwa kuwaondoa wale woote ambao jamii inawajua bila shaka yeyote ni mafisadi! Hatua anazozichukua Maguli ni njema kabisa, na zimedhoofisha upinzani bila ya siasa yeyote!

Acha kutishia watu Gurumo kwa vipande vya dinari ulivyochukua, hakuna aliemkuu kuliko chama, tumuunge Magufuli mkono kwa kumsadia na siyo kumkatisha tamaa kila uchwao kwa ngonjera zenje sumu ya maneno matamu!

Viva JPM, wanaopiga kelele ni wote wale wanao hofia nafsi na matumbo yao!
 
Chama cha MAJIPU
 
magufuli si mtu wa maneno,tusubiri na wewe ukae usubiri atakayoyafanya,tuombe mungu uzima............
 
Ndio mtindo wa ccm?

Ni wakina nani waliokuwa wanapiga kelele bungeni kuwa, "China huwa wanawanyonga mafisadi, na tunaomba rais asiwaonee haya mafisadi ikiwezekana awanyonge"..........Sasa hivi wanatumbuliwa, wanasema "Rais haangalii hakiza binadamu!"

Ukiibu hapo juu, ntajibu kama huo ni mtindo wa CCM au la!
 
Mpaka mahakama iwadhibitishe kua nimafisadi siyo kukurupuka
 
Kwa nini Mleta Mada, usitumie muda wako kufanya utafiti zaidi kwamba ni wapi hasa UKAWA mlijikwaa, na bado mkiendelea kuumizwa na kasi ya Magufuli?
Wewe ansbert ngurumo ni mmoja wa wagombea mliokosa majimbo Uchaguzi uliopita hivyo ungejikita zaidi kuuchambua mustakabali wa UKAWA chini ya Lowassa kuliko kulijadili CCM chini ya Magufuli ambako wewe si Mwanachama

Ungekuwa na chembe ya AKILI ungeshambulia hoja ya Ngurumo badala ya kumshambulia Ngurumo as a person.

SIMPLE MINDS DISCUSS PEOPLES
 
Uboya mtupu, we sema hiv "magufuli endelea kutumbua mafisadi yaje kwetu upinzani" na mtawasomba kwel kwel, mpaka boss atoke kuchunga n'gombe
Ficha upumbavu wako jadili hoja iliyopo, Kuna kashfa nyingi za ufisadi rada, mikataba ya madini, IPTL, EPA, ESCROW, meremeta, UDA na nyinginezo kibao zilizotengenezwa na kukumbatiwa na kulelewa na CCM, wahusika wamehamia upinzani?

Magufuli mwenyewe jipu, na jipu kuu Riz 1na babaake hathubutu kuingia kwenye anga zao, mmebakia majuha ya lumumba na buku 7 kukariri upuuzi
 
boya kabisa!

Ni habari yenye lengo la kufitinisha! N mwaandishi anaonyesha wazi kufanya kazi hii maluumu kwa kutumwa na watu maalumu, na hasa ili kujenga hofu kwa mtumbuaji!

Kuna wanachama na baadhi ya viongozi waandamizi wanajiona wao ndio CCM na kwamba kuguswa wao ama ufisadi wao, ni kukigusa chama! CCM siyo mtu ama genge la watu hasa wahuni na wahujumu wa uchumi!

CCM kimepoteza wanachama wengi na hasa imani kwa wananchi kutokana na wahuni wachache wanaojiona wenyewe ndio Chama Cha Mapinduzi! Na imlikuwa ni vigumu sana kukinadi chama kwa jinis vile kilinuka katika uchaguzi uliopita! Wananchi walikichoka!

Ili kukiimarisha Chama, ni lazima haki itendeke na Haki hiyo ionekane inatendeka mbele ya jamii kwa kuwaondoa wale woote ambao jamii inawajua bila shaka yeyote ni mafisadi! Hatua anazozichukua Maguli ni njema kabisa, na zimedhoofisha upinzani bila ya siasa yeyote!

Acha kutishia watu Gurumo kwa vipande vya dinari ulivyochukua, hakuna aliemkuu kuliko chama, tumuunge Magufuli mkono kwa kumsadia na siyo kumkatisha tamaa kila uchwao kwa ngonjera zenje sumu ya maneno matamu!

Viva JPM, wanaopiga kelele ni wote wale wanao hofia nafsi na matumbo yao!
Upinzani umedhoofika kivipi? Hadi leo rejea kauli ya prof Tibaijuka (ingawa wengine hawataki kujadili kauli yake bali wanamjadili yeye binafsi ) kuwa Magufuli anakamua nyama na si majipu.

Moyo wa majipu unajulikana, ni viongozi wakuu wa CCM, maana katika kila ufisadi mkubwa nyuma yuko mwanasiasa nguli wa CCM, Magufuli anajua ila anatafuta umaarufu kwa watumishi wa serikali.

Tumbua waliofanya utapeli wa IPTL wale waliofungua kampuni ya simba trust ya Australia wanaohusika na familia ya mzee wa Msoga.

Tumbua waliojigawia shirika la UDA kimagumashi.

Bila hivyo tuacheni wenye jicho la tatu tusiovutwa na ushabiki bali tu nasubiria majipu na si nyama
 
Mwili wa binadamu una sehemu tofauti tofauti.
Kuna sehemu rahisi hata kuzikata na kuzitoa bila kuleta athari kubwa za kiafya.

Jipu linapotokea kwenye mwili wa binadamu linauma sana. Maumivu yanakua makali zaidi kulingana na sehemu ya mwili lilipotokea.
Kuna baadhi ya sehemu za mwili wa binadamu zinauma sana zinapotokwa na jipu.
Mfano jipu likitokea Puani,kwenye sikio, sehemu za siri, tumboni ,kwenye jicho n.k. linauma sana sana.

Jipu linalotokea sehemu inayouma sana pia linakua ni vigumu kulitumbua kwa haraka bila utaalam wa ziada. Ukicheza nalo linaleta madhara makubwa zaidi.

Mfano likitokea jipu mkononi au kwenye paja la mguu inakua ni rahisi kulitumbua ukilinganisha na sehemu kama kwenye sikio.

Ni kweli kuwa Magufuli bado hajatumbua majipu yaliyoliyolisababishia taifa hili maumivu makali sana sana. Lakini hiyo isiwe sababu ya kukejeli kazi aliyoianza ya kutumbua baadhi ya majipu yaliyoko sehemu nyepesi kutumbua bila madhara makubwa.

Kazi aliyoianza ni nzuri lakini pia inapunguza idadi ya majipu yaliyoko kwenye taifa letu.
Ninaimani kuwa mwisho wa yote itabidi tu atumbue na yale majipu yanayolisababishia taifa letu maumivu makali sana. Asipofanya hivyo maumivu haya yataendelea kwa muda mrefu.

Ni lazima majipu yote yatumbuliwe bila kujali umuhimu wao kwenye kununua kura za wabunge wa CCM kupata ushindi wa kishindo bungeni. Hatuhitaji kuongozwa na bunge la wala rushwa. Wabunge na madiwani wengi wa CCM ni matokeo ya majipu na ufisadi wa kupata fedha za kununua nafasi hizo za uwakilishi hasa pale wasipokubalika.

Ni vizuri Magufuli akasafisha wale wakuu wa taasisi za umma na wafanyabiashara wanaotumiwa na mafisadi ndani ya vyama vya siasa ili kupata ubunge na baadae uwaziri.
 
Back
Top Bottom