Majipu yanayotumbuliwa na Magufuli...

Majipu yanayotumbuliwa na Magufuli...

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,802
Reaction score
50,393
Kuna chereko chereko nyingi sana toka kwa wananchi wengi kuhusu matendo ya Rais Magufuli anapoonesha kwamba anapambana na ubadhirifu na ufisadi uliotamalaki ndani ya Serikali. Matendo hayo ambayo yeye mwenyewe Rais ameyabatiza jina la "kutumbua majipu" na pia kujipa kazi ya "mtumbua majipu" bila shaka ni muendelezo wa kauli mbiu yake ya "Hapa kazi tu".

Lakini swali la kujiuliza hayo yanayoitwa majipu yalitokeaje tokeaje mpaka yakafika kuja kutumbuliwa na Magufuli? Maana majipu chanzo chake ni uchafu au mchafuko wa ndani ya mwili, kwa haya majipu anayotumbua Magufuli chanzo chake ni nini hasa?

Je chanzo chake ni uzembe wa Uongozi uliopita chini ya Marais Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete au chanzo ni Mfumo wa uendeshaji wa mambo ndani ya serikali, au chanzo kikuu ni Chama kilichotoa Marais Kabla ya Magufuli kuwa Rais?

Majipu yakitumbuliwa bila chanzo chake kushughulikiwa au kujulikana huko mbele ya safari si yatarudi tena? Majipu ni watu au ni mfumo unaoleta majipu? Kwa mfano yule Mkurugenzi wa Muhimbili aliyeomba hela za kukarabati mashine za CT Scan na hakupewa, yeye ndiye jipu au waliomnyima hela ndiyo jipu?
 
Bila shaka ni uongozi mbaya wa chama tawala kila baada ya miaka10 kauli mbiu hubadilika lakini utendaji Kazi hubaki palepale ni mwendendelezo tu was uozo uliotunukiwa na matokeo ya kubweteka
 
Vitu vingi sana husababisha matatizo ya ufisadi na wizi na matumizi mabaya ya ofisi za serikali, kwa kiswahili cha awamu ya tano linatumika neno majipu kumaanisha mambo yote hayo.

Uwezo mdogo wa maofisa wanaopewa ofisi kubwa za kiserikalini, wanakuwa mzigo na mambo mengi ya kitaalam yanawapiga chenga, matokeo yake wale wanaokuwa chini yao wanaichukulia nafasi hiyo katika kuiibia serikali kwani wanajua bosi mkubwa yupo kwenye cheo chake lakini ni "mtupu" kiuwezo.

Kulipa fadhila, kwa maana ya mtu anapewa cheo fulani serikali na mtu fulani, hivyo muda wote wa uwajibikaji wake anakuwa yupo kwenye mchakato wa ulipaji wa fadhila kwa yule aliyempigania mpaka akapata cheo alichonacho. Huyu aliyepiganiwa mpaka akawa bosi anakuwa ni mateka wa yule aliyempa ulaji, wanakula pamoja, wanatengeneza networks chafu za ulaji.

Kuna ile tabia ya mtu kutazamwa katika mtazamo wa kuingilia riziki za watu. Wapo wataalam ambao wanafanya interview vizuri sana, maprofesa wa vyuo vikuu wanasimamia interview wanaukubali uwezo wao. Majina yanapelekwa Ikulu, kiongozi mkuu wa awamu ya nne anawakubali na anarudishia faili kwa katibu mkuu wa wizara, huyu katibu mkuu kwa sababu anakula na yule mtu ambaye anakaimu ukurugenzi, anaamua kulificha lile faili ili lisimfikie waziri mwenye dhamana ya kukubaliana na ujumbe uliotoka kwa rais. Yaani katibu mkuu wa wizara na kaimu mkurugenzi wote wawili wanakuwa ni tatizo kwani wanamnyima mtu mwenye uwezo na sekta husika ile nafasi ya kuitumia elimu kwa faida. kwa hiyo mitandao kama hiyo ya urafiki na yenyewe imekuwa ikichangia katika uwepo wa majipu kila siku ndani ya mfumo wa uongozi.

Zipo sababu nyingi zinazosababusha uibukaji wa majipu, wakati mwingine tamaa za kibinadamu. Mtu anatamani kuw ana nyumba kama ile ambayo anaiona kila siku asubuhi pale Mbezi Beach wakati akipita na gari yake kutokea Tegeta akielekea ofisini posta mpya. Hiyo nyumba anayoiona thamani yake ni shilingi milioni 500, ili aweze kuijenga kwa pato lake, haiwezekani, hivyo kinachofuata ni kuchora michoro ya wizi.

Nadhani hizo ni baadhi tu ya sababu zinazochangia uwepo wa majipu ndani ya serikali, ndani ya awamu zote tano.
 
Majipu haya yametokana na mfumo wetu wa maisha tuliouchagua na CCM wamejinufaisha nao tu.

Hakuna asiyejua kutoa rushwa ni kinyume na sheria lakini tumefanya ndio utaratibu iwe hospitali au barabarani.

Tunakoishi hata utunzaji wa mazingira unatushinda, taka zinatupwa ovyo, mitaro inaziba na sisi tunasubiri viongozi wachukue hatua.

Angalia asilimia kubwa ya wabunge na madiwani ni watu wa aina gani ndio utaelewa sisi kama jamii tupo wapi.

CCM hawakuwahi kuona umuhimu wa kubadilisha hali hii waliamua kujinufaisha na kuacha watu waishi vile walivyozoea.

Hii haiwaondolei lawama vyama vingine kwasababu kama vyama vya upinzani nia yao ni kushika dola kwanza. Wangeweka dhamira ya kubadilisha fikra zetu kwanza leo wengine ndio wangekuwa watawala.

Mwanasiasa yupo tayari kuwatetea wamachinga wasifukuzwe wanapofanya biashara maeneo yasiyo rasmi lakini hata siku moja hutamuona akiwaelimisha umuhimu wa kufanya biashara maeneo rasmi na kuhakikisha wanapatiwa maeneo hayo na kupata haki zao za msingi.
 
Vitu vingi sana husababisha matatizo ya ufisadi na wizi na matumizi mabaya ya ofisi za serikali, kwa kiswahili cha awamu ya tano linatumika neno majipu kumaanisha mambo yote hayo.

Uwezo mdogo wa maofisa wanaopewa ofisi kubwa za kiserikalini, wanakuwa mzigo na mambo mengi ya kitaalam yanawapiga chenga, matokeo yake wale wanaokuwa chini yao wanaichukulia nafasi hiyo katika kuiibia serikali kwani wanajua bosi mkubwa yupo kwenye cheo chake lakini ni "mtupu" kiuwezo.

Kulipa fadhila, kwa maana ya mtu anapewa cheo fulani serikali na mtu fulani, hivyo muda wote wa uwajibikaji wake anakuwa yupo kwenye mchakato wa ulipaji wa fadhila kwa yule aliyempigania mpaka akapata cheo alichonacho. Huyu aliyepiganiwa mpaka akawa bosi anakuwa ni mateka wa yule aliyempa ulaji, wanakula pamoja, wanatengeneza networks chafu za ulaji.

Kuna ile tabia ya mtu kutazamwa katika mtazamo wa kuingilia riziki za watu. Wapo wataalam ambao wanafanya interview vizuri sana, maprofesa wa vyuo vikuu wanasimamia interview wanaukubali uwezo wao. Majina yanapelekwa Ikulu, kiongozi mkuu wa awamu ya nne anawakubali na anarudishia faili kwa katibu mkuu wa wizara, huyu katibu mkuu kwa sababu anakula na yule mtu ambaye anakaimu ukurugenzi, anaamua kulificha lile faili ili lisimfikie waziri mwenye dhamana ya kukubaliana na ujumbe uliotoka kwa rais. Yaani katibu mkuu wa wizara na kaimu mkurugenzi wote wawili wanakuwa ni tatizo kwani wanamnyima mtu mwenye uwezo na sekta husika ile nafasi ya kuitumia elimu kwa faida. kwa hiyo mitandao kama hiyo ya urafiki na yenyewe imekuwa ikichangia katika uwepo wa majipu kila siku ndani ya mfumo wa uongozi.

Zipo sababu nyingi zinazosababusha uibukaji wa majipu, wakati mwingine tamaa za kibinadamu. Mtu anatamani kuw ana nyumba kama ile ambayo anaiona kila siku asubuhi pale Mbezi Beach wakati akipita na gari yake kutokea Tegeta akielekea ofisini posta mpya. Hiyo nyumba anayoiona thamani yake ni shilingi milioni 500, ili aweze kuijenga kwa pato lake, haiwezekani, hivyo kinachofuata ni kuchora michoro ya wizi.

Nadhani hizo ni baadhi tu ya sababu zinazochangia uwepo wa majipu ndani ya serikali, ndani ya awamu zote tano.
Udini ndiyo uliutawala sana. bila kujali uwezo wa utendaji magufuli tunakuomba ukague idara zote
 
Udini upo ni kweli kabisa. Miaka kumi ya rais mkristo basi wakristo wanakuwa na ushawishi serikalini. Miaka kumi ya muislam waislam wanakuwa na sauti kwenye jamii. Huu ni ufa ambao tumeshindwa kuuziba.
 
Back
Top Bottom