Majina ya Kinyakyusa na maana zake, twenzetu hapa

Ambilikisye : Amenisikia
Ahombile:???
Mbonile:???
Mboka:???
Bupe:???
Lwitiko:Imani
Asumwisye:???
Nsubili:???
Ndimyaki
Ndimyaki........nipo kwake
asumwisye.......ameniamsha
mboka.........nisaidie
ahombile..........amelipa fidia
 
Angalizo: neno moja la Kinyakyusa linawezakuwa na maana tofauti kulinfana na unavyolitamka. Ukilivuta neno huleta maana tofauti na ukilitamka kwa haraka. Mfano Anyagile inawezakuwa AMENIPTA ukilivuta (Anyaagile) au AMENIROGA (Aanyagile) au AMEROGA (Anyagile)
Hakika mkuu,hata mazingira pia yanaweza kutoa maana ya neno la kinyakyusa,upo sahihi
 
MAJINA YA KINYAKYUSA NA MAANA YAKE.

LUSAKO. BAHATI
LUSAJO. BARAKA
LUGHANO. UPENDO
LUTENGANO. AMANI
LUSEKELO. FURAHA
LUSUBILO. TUMAINI
TUPOKIGWE. TUMEOKOLEWA
TUPOKE. TUOKOE
MPELI. MUUMBA
NTULI. MSAIDIZI
NTOLI. MSHINDI
MPOKI. MUOKOZI
MBUTOLWE. SHIDA
KISSA. HURUMA
ULIMBOKA. NIOKOE
ANDINDILILE. AMENILINDA
ASUMILE. ALIOMBA
ANGANILE. ANANIPENDA
ATUGANILE. ANATUPENDA
ATUFIGWEGE. ASIFIWE
ANYISISILE. AMENIJIA
AFWILILE. ALINIFIA
AHOBOKIILE. AMENISAMEHE
ASAJILE. AMENIBARIKI
ANYOSISYE. AMENIBATIZA
ANYELWISYE. AMENITAKASA
NDIMBUMI. NIPO UZIMANI
NDIMBWELU. NIPO KWENYE NURU
ATUPELE. AMETUPA
TUMPALE. TUMSIFU
NELUSIGWE. NIMEBATIZWA
NTUFYE. MSIFU
GWANTWA. MWANA/ MTU WA MUNGU
GWAKISA. MWENYE HURUMA
GWAMAKA. MWENYE NGUVU
GWANDUMI. MALAIKA
TISEKIILE. TUMEFURAHI
SEKELA FURAHI
IPYANA. HEKIMA
ATUPAKISYE. ANATUJALI
USWEGE. UNISAMEHE
ANDONGWISYE. AMENIONGOZA
AMBWENE. AMENIONA
GWALUGANO. MWENYE UPNDO
MJE MASO. MUWE MACHO
NEGWAKO. NI WAKO
ANDWELE. AMENILETA
ANDOBWISYE. AMENIVUSHA
TUSAJIGWE. TUMEBARIKIWA
LUTUFYO SIFA
ANGUMBWIKE. AMENIKUMBUKA
AMBILIKILE. AMENISIKILIZA
AMBINDWILE. AMENIBADILI
AMBELE. AMENIPA
AMANYISYE. AMENIFUNDISHA
AMULIKE. AMENIANGAZA
LUMULI NURU
LUBATIKO. UTARATIBU
SUBILAGA. TUMAINIA
ANGETILE. AMENITAZAMA
ANDONDILE AMENITAFUTA
ANGANILE. ANANIPENDA
ANGOLWISYE. AMENINYOSHA
ANDOGWISYE. AMENIONGOZA
NSAJIGWA MBARIKIWA
NKUNDWE. MPENDWA.

HAYA NI BAADHI YA MAJINA YA KINYAKYUSA NA MAANA YAKE, ASILIMIA KUBWA YA MAJINA HAYA YAMEBEBA SIFA NA UTUKUFU WA MUNGU, PENDA MAJINA YA ASILI YAKO USIWE MTUMWA WA MILELE.

ULIZA JINA UNALOLIJUA LAKINI HUJALIONA HAPO WANAOFAHAMU MAANA YAKE WATAKUJA KUKUJIBU.

NAKUTAKIA SIKU NJEMA MTU WA MUNGU



Mkuu, mimi siyo Mnyakyusa, lakini umenipa somo zuri sana kutokana na post yako hapa, ipo haja ya kuanzisha jukwaa lenye sub platforms za lugha zetu za asili, hiyo itasaidia sana:

1. Wale waliokulia mijini kujifunza lugha za asili yao kwasababu lugha za asili zinaanza kufutika polepole

2. Mwingiliano wa makabila katika kuoleana na kuishi na kufanya kazi pamoja kama watanzania, siyo vibaya kujifunza na kujua lugha ya jirani yako ili kuimarisha udugu na ujirani mwema, mfano mchagga akienda Mbeya basi ajue hata sentesi ya kuombea maji, hiyo itamfanya mnyakyusa kujisikia ana ndugu mchagga anayejali lugha yake

Hongera Mkuu kwa somo la leo
 
Mwambile, Mwakalinga, Mwakisunga, Mwakisopile.

Maana yake mheshimiwa tafadhali.
 
Back
Top Bottom