Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

NA BABU APEWE JAPO KIDOGO.

Niliona gari limeandikwa hivyo, nikawaza sana
 
Wakuu ni vipi?

Katika pita pita zangu nakuwa nikikodolea macho mabango yaliyoandikwa kwenye vyombo vya usafiri kama daladala, bajaji, pikipiki n.k

Sasa nikaona sio vibaya tukaanza kushare yale maneno humu kila tunapoyaona.

Naanza mimi:

"Ikiwaka mulika"

"Kama hujaoga huendi mjini na sisi"

Tupia chako.
 
Uzi Kama huu uliwa kuwepo ulijaa maneno ya kwenye usafiri Kama,
huu,👇

Mawe yataiva Kuni zitabaki,

Uzi huo kwasasa una misemo kuliko usafiri aina zote😂

Mods ,hawatachelewa kuunganisha nyuzi zote mbili ...
 
Jamani hapa bongo utakutana na daladala zina majina kiboko,mimi natupia baadhi nawe tupia yako hapo chini.

1. Majungu mliyoyapika sasa mtayapakua
2. Nenda kaseme tena
3. Gusa unate
4. Flag ya chuma
5. Masikini hafilisiki
usilale kesho marejesho
Mwambie mkeo gari sio yangu
Tatizo tochiii
 
Wakuu ni vipi?

Katika pita pita zangu nakuwa nikikodolea macho mabango yaliyoandikwa kwenye vyombo vya usafiri kama daladala, bajaji, pikipiki n.k

Sasa nikaona sio vibaya tukaanza kushare yale maneno humu kila tunapoyaona.

Naanza mimi:

"Ikiwaka mulika"

"Kama hujaoga huendi mjini na sisi"

Tupia chako.
Yangu macho.
 
..
IMG_20210303_215840.jpg
 
Back
Top Bottom