Majina na michango msibani

Majina na michango msibani

nandembako

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
655
Reaction score
528
Labda leo nijiulize kwenu wadau,maana halisi ya kuandika jina unapotoa mchango wa msiba...nawaza jina linaandikwa ili kiwe nini,kwamba ulikuwepo au kuna mahali waliotoa wanaandikwa kwa kumbukumbu....ninachoamini msiba sio sherehe unapoweka daftari mtu akaandika anajishtukia kutoa alichopanga kukitoa pengine anaweza kuona kidogo watamshangaaa au kikubwa watu watamuona anajidai...ni mtazamo tu

by emma mjasiriamali
 
Ili kama jina lako halipo bhasi utarajie kutokuchangiwa siku yakikukuta na wewe
 
Sasa hivi mitaa mingi ina daftari la michango ya msiba, Pindi utokeapo msiba linapitishwa nyumba kwa nyumba utakachotoa unaandika jina lako.

Ili siku nawe umepatwa na shida wanaangalia kama huwa unatoa kwenye matatizo ya wenzio.

Mimi naona ni utaratibu mzuri ni kama kumtisha mtu atoe mchango kilazima ili afikirie na yeye akipata shida wasije kugoma kutoa.
 
Hiyo ni kanuni ya pesa worldwide, kwa watu makini pesa inapotolewa au kutumika ni muhimu iambatane na uwekaji wa kumbukumbu ili iwe rahisi kuhakiki, kwa dunia ilivyo palipo na harufu ya pesa wapigaji nao huwa hawachezi mbali,kumbukumbu inasaidia kuhakiki kama kiasi kilichokusanywa hapo msibani kinaendana na kiasi halisi kilichochangwa na watu,vinginevyo wanaweza wakaja watu kumi kila mmoja amechanga elfu kumi lakini kwa kuwa hakuna record muhusika hapo mezani badala ya kuwasilisha laki moja akawasilisha sh. elfu kumi nyingine akatia mfukoni.
Hata hivyo huwa hakuna anayekulazimisha kuandika jina unapotoa kama hupendi kuandikwa,kwani wapo ambao imani zao zinawaelekeza mkono wa kulia unapotoa hata mkono wa kushoto hautakiwi kujua sembuse mwanadamu mwingine,so unaweza kuweka milioni yako bila kuandika na kama unajitambua hakuna wa kukulazimisha kuandika jina.
 
Back
Top Bottom