Majimbo yasio na uwakilishi bungeni

Majimbo yasio na uwakilishi bungeni

Inkoskaz

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
6,360
Reaction score
2,389
Tuna baraza la mawaziri na manaibu wao wanaokaribia sitini na wengi wakiwa ni wa kuchaguliwa na wananchi kuwawakilisha kutoka katika majimbo yao
Sidhani kama kama kila waziri alijua kuwa atateuliwa baada ya kushinda ubunge na sidhani kama kila wananchi walijua kuwa mwakilishi wao ataukwaa uwaziri baada ya wao kumchagua kwa preference zao na mategemeo fulani nyuma yake

Swali la kujiuliza;
Baada ya muwakilishi kuukwaa uwaziri na kuhamia makao makuu ya serikali(DAR) na kuripoti wizarani kwake kila siku nakufanya kazi za serikali ni nani anabaki kuwakilisha wananchi wa jimbo lake?

mfano jimbo liwe na kero ya maji halafu mbunge huyohuyo akateuliwa kuwa waziri wa maji nani atawasemea wapiga kura wake? Na akiamua kulitafutia ufumbuzi si ataonekana amependelea jimbo lake kwa wadhifa na madaraka aliyopewa?
Nani anahudhuria vikao vya madiwani na vingine vya halmashauri a mbunge kwa nafasi yake huingia moja kwa moja?

nani husikiliza kero na malalamiko au maoni ya jimbo lake wakati yeye hayupo? Ufuatiliaji wa miradi jimboni kwa kila hatua itafanywa na nani kama si kuishia kupewa taarifa fake?

Hebu jenga taswira majimbo sitini ukiongeza na la spika na naibu wake hayana uwakilishi.najua wapo viti maalumu lakini kundi hili liawakailisha baadhi ya kada na si chaguo la wanachi wote hivyo bado pengo ni dhahiri

Pia hawa wakuu wa mikoa na wa wilaya ambao ni wabunge wakuchaguliwa majimboni ni mapungufu makubwa katika mfumo kwani hata mgongano wa kiutendaji ni lazima utokee..kwani hakuna wanachi wengine wenye sifa mpaka kumpa mtu kofia mbilimbili? Are we serious?

Watanzanie tuamke,tusio na wawakilishi tudai wawakilishi....

Kivipi??? Tuhakikishe uwiano katika mabaraza ya katiba na bunge la katiba ili tupate KATIBA yenye nia yakumkomboa kila mtanzania
 
Mbona WENJE anataka kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo hajatangaza kutokugombea Nyamagana?
 
Chadema unataka nicheke; mawaziri kivuli, Sugu, Zitto, Lissu na Mbowe wanaishi DSM mbona hauhoji???
 
Sisi wa jimbo la kyerwa pamoja na kwamba tuna mbunge lakini si mwakilishi ijapokuwa hakupewa uwaziri hujikalia dar na akiingia bungeni uwa kama waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa yaani observer hachangii chochote
 
Chadema unataka nicheke; mawaziri kivuli, Sugu, Zitto, Lissu na Mbowe wanaishi DSM mbona hauhoji???
Ni mambo mawili yasiyofanana kabisa!

wanakuwepo Dar kwa shughuli za bunge na za kichama hivyo kuwa na makazi si kosa na pia hwana ofisi wanazotakiwa kuripoti kila asubuhi kwa siku za kazi kama ilivyo kwa mawaziri ambao wanalazimika kuwa na makazi ya kudumu,ofisi ya kudumu na job description inayoeleweka ambayo inawabana kutumikia majimbo

nadhani uwaziri, u-RC,u-DC na watendaji wa mtaa ni kazi pekee za kisiasa zinazolipiwa mshahara na serikali
tuweke mawaziri wasio wabunge
tuondoe maRC na maDC
 
Sisi wa jimbo la kyerwa pamoja na kwamba tuna mbunge lakini si mwakilishi ijapokuwa hakupewa uwaziri hujikalia dar na akiingia bungeni uwa kama waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa yaani observer hachangii chochote
kakimbia Karagwe? hakika wabunge wasichangia hata kwa mara moja au kuuliza maswali wanasikitisha wapiga kura wao.Japo kuna utaratibu wa maandishi lakini inajulikana wazi hoja za kuongea zina mashiko na hufuatiliwa kwa karibu na wengi
 
Chadema unataka nicheke; mawaziri kivuli, Sugu, Zitto, Lissu na Mbowe wanaishi DSM mbona hauhoji???
Hoja yangu Uchama umetoka wapi MAFILILI? hebu ndugu tujivue ukabila,udini,jinsia,itikadi za vyama nk tuongelee utaifa wenye manufaa kwetu sote
 
Last edited by a moderator:
naunga mkono hoja katiba ijayo hawa watu wawe wanachaguliwa na wananchi haya maoni nilitoa kwa tume ya warioba na dr salim.
 
Majimbo kama ya Tundu Lissu, Msigwa, Sugu, Wenje, Selasini, hayo ni majimbo yasiyo na wawakilishi na lazima yarudi CCM kama hautaki andamana.
 
naunga mkono hoja katiba ijayo hawa watu wawe wanachaguliwa na wananchi haya maoni nilitoa kwa tume ya warioba na dr salim.
Huo ndio muafaka bila kuwa na taasisi inayotoa leseni baada ya mafunzo kamili basi madereva watakuwa wanatusababishia ajali tu kila siku
 
Lema................................?
Majimbo kama ya Tundu Lissu, Msigwa, Sugu, Wenje, Selasini, hayo ni majimbo yasiyo na wawakilishi na lazima yarudi CCM kama hautaki andamana.
 
Majimbo kama ya Tundu Lissu, Msigwa, Sugu, Wenje, Selasini, hayo ni majimbo yasiyo na wawakilishi na lazima yarudi CCM kama hautaki andamana.
Atubela hilo sahau
pia tambua kuna todfauti ya mbunge na mbunge waziri...kwa mfano waziri wa foreign affairs anamuwakilisha raisi safari hata mikutano mingi kwa niaba.je attacha jukumu hilo aende jimboni kwake hata kama kuna nyumba zinachomwa?
 
Last edited by a moderator:
Majimbo kama ya Tundu Lissu, Msigwa, Sugu, Wenje, Selasini, hayo ni majimbo yasiyo na wawakilishi na lazima yarudi CCM kama hautaki andamana.
Hakuna mtu anaandamana maana janja ya nyani kwsa jua!! Ni kipigo kimya kimya tu kama mlivyoona jana Kilosa na kuendelea
 
Back
Top Bottom