Majigambo ya Zitto yawachefua CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majigambo ya Zitto yawachefua CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 30, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe jana alikera wabunge wa CCM wakati alipotumia muda mwingi kusifia mafanikio yake jimboni lake katika kipindi cha miaka mitano.

  Zitto, ambaye alikuwa akizungumza kama msemaji wa kambi ya upinzani katika Wizara ya Miundombinu, alitumia zaidi ya dakika 10 kujimwagia sifa na kujipambanua kuwa ni mbunge bora kuliko wabunge wote wa mkoa wa Kigoma, kitu kilichoonekana kuwakera watunga sheria wengine kutoka mkoa huo na mmoja wao kulazimika kuomba mwongozo wa spika.

  “Kwa wabunge wa Kigoma tofauti na mimi na kwa michango yao iliyochochea maendeleo ya mkoa wetu wa Kigoma, Mungu atawalipa. Lakini siwaombei mrudi bungeni kwani ni lazima kuimarisha demokrasia ya vyama vingi kwa kuchagua wabunge wengi zaidi wa upinzani... na mkoa wa Kigoma ni muhimu na lazima kupata wabunge wengi kutoka kambi ya upinzani ili kupaza zaidi sauti ya Kigoma jambo ambalo wabunge kutoka CCM wanakwazwa,” alisema Zitto

  “Hata hivyo tutawakumbuka katika historia kama wabunge mliokuwapo katika miaka muhimu ya mabadiliko katika mkoa wa Kigoma na Mungu awajalie huku mwendako!”

  Katika maelezo yake Zitto alisema jimbo la Kigoma Kaskazini na mkoa wote wa Kigoma umepata maendeleo makubwa katika kipindi hicho ambacho yeye ni mwakilishi bungeni.

  Kauli ya Zitto ilimchefua mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Selukamba ambaye aliomba mwongozo wa spika na kueleza kuwa mafaniko yote yaliyopatikana jimboni kwa Zitto ni utekelezaji wa sera za chama tawala, na sio jitihada zake kama mbunge.

  “Mheshimiwa Spika napenda kulieleza Bunge lako kuwa mafaniko yote anayoyaeleza mheshimiwa Zitto hayakupatikana kwa nguvu zake bali ni utekelezaji wa sera ya CCM,” alisema Selukamba.

  Lakini Spika Samuel Sitta alimjibu akisema: “Mheshimiwa mbunge usingetegemea mbunge wa upinzani asimame hapa na kuisifia CCM. Kikubwa tu serikali ingekuwa makini maana mambo yote hayo kama yanapelekwa kwenye jimbo moja tu tena la upinzani, hii ni hatari.”

  Spika Sitta alimtaka Zitto ajiunge na CCM kwa kuwa ana mvuto maalumu ambao uliishawishi serikali kuboresha miondombinu hasa ya barabara na umeme.

  “Ukweli ni kwamba Kabwe ana mvuto maalumu na ndio maana serikali kupitia ilani ya CCM imediriki kuboresha mioundombinu ya barabara katika jimbo lake na Kigoma kwa ujumla,” alisema Sitta wakati Zitto alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani.
  “Umesema mambo mazuri sana Mheshimiwa Zitto, lakini tatizo lako umeng'ang'ania kukaa katika vyama vya upinzani. Njoo CCM.”

  Awali akiwa anaelezea maeneleo ya Kigoma, Zitto alisema anawashukuru wakazi wa jimbo lake kwa ushirikiano mkubwa waliompa na hata kuwezesha maendeleo ambayo sasa yamefikiwa.

  “Mwaka 2005 kulikuwa kuna mtandao wa barabara za lami wenye kilomita nane tu kwa mkoa mzima wa Kigoma, leo kuna mtandao wenye kilomita 80 na ikikapo Oktoba mwaka 2010 kutakuwa na mtandao wenye kilomita zaidi ya 100,” alisema mbunge huyo kijana.

  Zitto aliendelea kusema mwaka 2005 kulikuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 4 pekee za umeme pekee, lakini leo Kigoma ina uwezo wa kuzalisha migawati 11.

  Alisema mwaka 2005 Kigoma hapakuwa na gati hata moja katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, lakini sasa kuna magati mawili yanayoendelea kujengwa na mamlaka ya Bandari Tanzania- moja Kigoma Kusini na jingine Kijiji cha Kagunga jimboni kwake.

  “Mwaka 2005 hatukuwa na bweni hata moja la wanafunzi wa kike katika wshule za sekondari, leo Kigoma Kaskazini peke yake inajenga mabweni matatu katika shule tatu tofauti ili kuhakikisha mabinti wa Kigoma Kaskazini wanasomo bila matatizo," alisema.

  Alieleza kuwa wakati Rais Jakaya Kikwete anatembelea mkoa wa Kigoma ukiachana na miradi ya kimkoa aliyozindua, miradi mingine yote ilizinduliwa Kigoma Kaskazini peke yake.

  “Watu wa Kigoma Kaskazini wanajivunia sana maendeleo haya ambayo yametokea ndani ya miaka mitano tu. Mheshimiwa napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kutusikiliza watu wa Kigoma, hasa mimi binafsi nikiwa mbunge pekee wa upinzani kutoka mkoa wa Kigoma.”

  “Maneno aliyosema rais kuwa serikali haibugui maeneo kulingana na itikadi za vyama alipokuwa akizundua mitambo ya umeme Kigoma, ndio maneno ya kiungwana katika demokrasia yeyote duniani.”

  Akizungumzia maoni ya upinzani katika bajeti ya Miundombinu, Zitto alisema wizara hiyo ni mzigo kwa serikali kwa kuwa imeshindwa kutekeleza mambo mengi muhimu yaliyoelezwa katika ilani ya CCM.

  chanzo Majigambo ya Zitto yawachefua CCM

  CCM Safari hii imepata Upinzani bungeni hongera Mbunge kijana Mh Zitto.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni kweli tukiwa na wabunge 20 kama akina zitto, Dr Slaa, Said arfi, Halima mdee, n.k. nchi inaweza kusogea
   
 3. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Lakini Spika Samuel Sitta alimjibu akisema: "Mheshimiwa mbunge usingetegemea mbunge wa upinzani asimame hapa na kuisifia CCM. Kikubwa tu serikali ingekuwa makini maana mambo yote hayo kama yanapelekwa kwenye jimbo moja tu tena la upinzani, hii ni hatari."
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Maigizo at best. Tumesema haya kila siku.

  Huyu anasem a nimeleta maendeleo, huyu anasema ni ilani ya CCM, mwisho wa siku ni kwamba hawa watu tunawalipa posho na mioshahara kwenda kufanya maigizo, is it really viable??
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Haiwezi kusogea mpaka wawe zaidi ya nusu ya wa CCM!
   
 6. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Nilisikia sehemu ya maelezo ya Zitto ingawa binafsi kilichonishangaza ni kutoa sifa zinazozidi kipimo kumusifia Kikwete. Sikuelewa maana sifa zingeelekezwa kwa serikali na siyo Kikwete kama alivyo ng'ang'ana. Nadhani aliingia kwenye mtego wa wana-CCM ambao huwinda uhusiano mzuri na Kikwete ili wakumbukwe. Sikujua lengo la Zitto.

  Kwa hilo la kusifia mafanikio yake sioni ajabu. Huko Bungeni baadhi ya wakuu na hasa Mawaziri huanza kusoma hotuba zao kwa kusifia wake zao, watoto na Mwandosya alifikia hatua ya kuomba samahani kwamba alisahau kuwataja waume wa watoto wake (wakwe).

  Kama kuna muda wa kuchezea kiasi hicho kwa nini mbunge asijisifu kwa masaa yote?

  Lakini pia huko Bungeni, mbona naona spika anaongoza Bunge kama mwenyekiti wa CCM? Nilidhani akiwa hapo kama spika anastahili kuwa ni mtu asiye na upande.
   
Loading...