Kutoka insta, Shigongo anadai kwamba umaskini ni laana ,na mafundisho ya dini yanasababisha umaskini huo kwa wakristo..
Majibu yangu
Erick Shigongo sio watu wote wanaweza kuwa na fedha za kutosha kama unavyodhani ,hakuna mahali katika biblia panaposemwa kwamba "Umaskini ni laana" hakuna kitu kama hicho ..
Yesu alisema Yohana 12 : 8 - kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamnami sikuzote...Na
Yakobo 1 : 27 -inasema kuwa dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu baba ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa. Na Yesu anaeleza kwamba kadiri tunavyowajali maskini ni kama tunamtendea yeye Mathayo 25 : 35 - kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha.
Erick Shigongo mungu huwabariki watu ili wawe mibaraka(mifereji ya kuwabariki) wengine, kama wenye fedha wakishindwa kuwahudumia wengine ambao ni maskini hawa ndio fedha huwa laaana kwao, lakini pia suala sio pesa au mtu kuwa na utajiri, bali suala ni namna gani unavyopata hizi pesa kama una fedha nyingi sana na njia uliyotumia kuzipata haipatani na njia ya mungu hiyo ndiyo laaana, na kwa kuwa wenye fedha wamejawa na kiburi na dharau, Yesu akasema "Ni vyepesi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu" luka 18 : 25
Aidha kusema kuwa mafundisho ya dini yanawafanya watu kuwa maskini hiyo nayo sio kweli, hakuna fundisho la dini ya kikristo linasema watu wawe wazembe Mungu mwenyewe alisema
Oka 20:8-11 ....... Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya bwana, Mungu wako.
Na mwenye hekima asema:Mithali 10 : 4 - atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
Cha kufahamu ni kwamba :Yesu hakuja dunia ili kuwafanya watu wawe matajiri au maskini bali alikuja kuwatoa katika dimbwi la dhambi, mchakato wa kutolewa katika dimbwi hili wakati mwingine una maumivu makali ikiwa ni pamoja na umaskini kutegemea na mtu
Utajili wako shingongo wa kuuza magazeti ya udaku ? Kuchezesha kamali watu ,hivi ndivyo vitu vya kutambia watu ?
Ongeza ufahamu hapa
Luka 16 : 19 - akasema, palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
Luka 16 : 20 - na maskini mmoja, jina lake lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi
Luka 16 : 21 - naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
Luka 16 : 22 - ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
Luka 16 : 23 - basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
Luka 16 : 24 - akalia, akasema, ee baba ibrahimu, nihurumie, umtume lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Luka 16 : 25 - Ibrahimu akasema, mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.