Majibu ya salamu za mwaka mpya

houseboy

Member
Jul 22, 2007
39
3
Asante sana Mheshimiwa Raisi wetu wa jamuhuri ya muungano kwa hotuba yako ya mwaka mpya,mimi kama mwananchi naomba nikujibu baadhi ya mambo uliyoeleza kwenye hotuba yako,na nitajibu kama ifuatavyo-
(1)CCM NA CUF ZANZIBAR.
Mh.Rais tatizo la Zanzibar linaweza kuleta matatizo makubwa sana katika nchi yetu,tangu tulipoanza mfumo wa vyama vingi na kufanya uchaguzi 1995 kumekuwa na malalamiko mengi sana kuhusu taratibu za uchaguzi,kama unakumbuka wananchi walikufa na tume zikaudwa,kutatua mgogoro huu,hakuna mtu anaweza kutatua mgogoro wa zanzibar isipokuwa wewe,na kwa ushauri wangu ningeomba usimamie kuunda serikali ya pamoja kwani hata matokeo ya uchaguzi yanapotoka mshindi uwa anashinda kwa %ndogo sana.
(2)UHALIFU UNAZIBITIWA.
Mh.Raisi katika hotuba yako umesema wahalifu wengi wamekamatwa na watuhumiwa wengi wa rushwa wamepelekwa kwenye vyombo vya sheria.katika swala hili mheshimiwa wahalifu wengi bado wapo wanaendelea kufanya uhalifu kila kukicha na wala rushwa wanaendelea uhalifu kama kawaida wakiongozwa na mapolisi wasio na uhadilifu ,si jambo la kufichika umejitaidi sana ulipowafikisha baadhi ya wahalifu,naomba katika mwaka huu usimamie kikamilifu kukabiliana na swala hili kuanzia maofisini mpaka kwa viongozi wasio wadilifu,jambo hili linawakela wananchi wengi sana na linatia nchi yetu umasikini mkubwa,wananchi wanapotaka uduma wanaambiwa watoe hela ya chai kwa huduma ya kawaida kabisa.
( 3)UCHUMI .
Mheshimiwa umesema mauzo ya mazao ya biashara yameshuka sana,na upungufu wa wawekezaji umechangia kutokua na uchumi mzuri,pia kudondoka kwa uchumi wa dunia,pia uchukuzi wa mizigo kutoka nchi yetu na nchi jirani ulipungua kwa asilimia kubwa.ni kweli kuhusu uchukuzi wa bidhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine umeathilika kutokana na wizi unaofanyika kutoka port zetu,bandari,Airport na reli,nchi kama Rwanda,burundi,Zambia,malawi kuna wakati walikua wanategemea kusafirisha vitu vyao kutoka bandari zetu walipoona ruswa,wizi wa vitu vyao na ushuru mkubwa wanaona bora watumie bandari ya Nairobi,msumbiji au SouthAfrica.pia umesema selikali imechukua mzigo wa madeni ya benki ya makampuni na watu waliopata hasara,hapo umekosea kabisa badala ya kuwapa au kuchukua deni hilo ungewapa wananchi mikopo midogodogo ili waweze kujinufaisha wenyewe,je makampuni na mabenki watarudisha walichopewa?.
(4)HALI YA MVUA NA CHAKULA.
Mh,Raisi mimi naona tusitegemee sana mvua,kwani tuna maziwa na mito yenye maji kabao tuwekeze katika kilimo cha umwagiliaji toboa ziwa victoria ,Tanganyika,nyasa,na mengineyo mengi miaka yetu mitano tu tunalisha Africa nzima,kila mwaka kuna upungufu wa chakula kwa sababu ya kusubiri mvua za vuri masika kukuza mazao yetu.
(5)MIUNDO MBINU.
Mh.miundo mbinu ni muhimu sana katika maendeleo ya taifa,tukitengeneza miundo mbinu mazubuti itakua simple sana kufanya maswala uchukuzi,utalii ni muhimu kuhakikisha barabara zetu zote zinakuwa kiwango cha lami tukianzaia kuunganiasha mikoa yote kisha wilaya na kumalizia vijijini .
(6)UMEME,
Mh.Raisi umezungumzia jinsi unavyojitaidi kutatua swala la umeme,mimi naona ni wakati umefika kuwekeza kwenye solar na wind,kwani umeme wa kutumia maji umepitwa na wakati na ni galama sana,vyuo vyetu vifanye utafiti wa kutengeneza solar na windi jua lililopo Tanzania linatosha kabisa kuendesha kila kitu.
Kwa kifupi ayo ni mawazo yangu ya majibu ya hotuba yako,mimi si mwandishi mzuri ni matumaini wasaidizi wako watasoma majibu haya kwa kifupi pia wana JF wataalamu watanisaidia kupanga au kuelezea kwa vizuri,asante sana Mh.Raisi wetu,asanteni wananchi wenzangu.mungu ibaliki TANZANIA NA WATU WAKE.
 
Back
Top Bottom