Majibu ndani ya Katiba CUF kuhusu Mgogoro ndani ya CUF. Lipumba amulikwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,493
54,900
SEHEMU YA KWANZA: [FACTS FINDING] Katiba ya CUF;-

Na. Maharagande,

Msingi wa Sera za CUF ni HAKI SAWA KWA WOTE. Kauli mbiu yetu asiyependa HAKI huwa tunasema kuwa AELIMISHWE. Hakika tumechukua jukumu hili la kuendelea kuwaelimisha wale wote wasiojua na au wasiopenda HAKI. Na wasipoelimika kwa maelezo haya WATANYOOSHWA NA VYOMBO VYA SHERIA-MAHAKAMA. Tumeupitia upuuzi wa Msemaji wa Lipumba alioandikiwa na Wakili wao. Kutokana Na [IQ-Intelligence Quotient] ndogo ya baadhi ya hawa wenzetu waliopata elimu kupitia Programu ya MEMKWA itabidi twende taratibu kwa muundo wa maswali na majibu [FACTS FINDING] ili dozi iingie uzuri na tunaanza kama ifuatavyo:

QUESTION NUMBER 1:

Je ni kweli katiba ya CUF ipo kimya kuhusu suala la kiongozi aliyejiuzulu kutengua kujiuzulu kwake?

COUNTER:

Hapana. Katiba ya CUF haipo kimya. Mamlaka ya KUTENGUA maamuzi yeyote yale yamewekwa ndani ya Katiba ya CUF Ibara ya 79. (1) wajibu wa Mkutano Mkuu wa Taifa utakuwa kama ifuatavyo:- (f) Kuthibitisha au KUTENGUA UAMUZI WOWOTE uliotolewa na kikao chochote cha chini
au KIONGOZI YEYOTE WA CHAMA.

QUESTION NUMBER 2:

Je ni kweli kuwa lipumba hakujiuzulu uenyekiti wa chama cha CUF kwa mujibu wa katiba ya CUF?

COUNTER:

Hapana sio kweli. Lipumba alijiuzulu Tarehe 5/8/2015 na akautangazia umma pale Peacock Hotel Tarehe 6/8/2015 kuwa ameng’atuka nafasi hiyo ya UENYEKITI na kubakia Mwanachama wa kawaida na kwamba kadi yake ameilipia mpaka mwaka 2020.

QUESTION NUMBER 3:

Ni nini kiini cha ‘mgogoro’ wa CUF?

COUNTER:

CUF haina Mgogoro wowote wa KIUONGOZI kwa mujibu wa Katiba yake na Sheria za nchi. Kilichopo ni NJAMA, HILA NA MIPANGO OVU inayoratibiwa na serikali ya CCM kwa kumtumia Lipumba na genge lake wakisaidiwa kwa uratibu maalumu na vyombo mbalimbali vya serikali ikiwemo TISS, Polisi, Jaji Mutungi na Ofisi yake ya usajili wa vyama vya siasa nchini, RITA, Spika na Bunge lake, Nakadhalika. Kinachofanyika ni kujaribu kuharibu taswira ya CUF, kudhoofisha uimara wa CUF, upinzani nchini pamoja na kujaribu kufifisha madai ya ushindi wa CUF wa Tarehe 25 Oktoba, 2015 Zanzibar.

QUESTION NUMBER 4:

Je Tarehe 5/8/2015 Lipumba aliandika barua ya KUSUDIO la kujiuzulu au aliandika barua ya KUJIUZULU?

COUNTER:

Lipumba hakuandika barua ya KUSUDIO LA KUJIUZULU. Aliandika BARUA YA KUJIUZULU. akachukua kila kilicho chake na kuondoka ofisini, Buguruni [QUIT FROM OFFICE].

QUESTION NUMBER 5:

Nini tofauti kati ya KUSUDIO LA KUJIUZULU na KUJIUZULU?

COUNTER:

KUSUDIO LA KUJIUZULU; [NOTICE OF INTENTION TO RESIGN] Ni kumjulisha muajiri wako nia ya kutaka kuacha kazi/nafasi huku ukiendelea na utekelezaji wa majukumu yako ya kazi ukisubiri majibu yake au tarehe ulioitaja kuwa IKIFIKA utakuwa umejiuzulu.

KUJIUZULU: [TO RESIGN ] - LEAVE YOUR JOB; Ni kuondoka na kuacha kabisa kutekeleza majukumu ya kazi/nafasi uliyokuwa unaitumikia.

QUESTION NUMBER 6:

Je katiba ya CUF inamkataza kiongozi asijiuzulu na kumtenza nguvu kuendelea na utumishi wake ndani ya Chama?

COUNTER:

Hapana. Ibara ya 117(1) inaeleza kuwa; “kiongozi yeyote wa chama anaweza kujiuzulu uongozi wake wakati wowote ule.”

Je wakati wowote maana yake nini? hata iwe kipindi cha uchaguzi mkuu wa nchi? NDIO ANARUHUSIWA. Hata kama baada ya siku 3 tangu achaguliwe? NDIO ANARUHUSIWA. Je hata iwe saa 8 za usiku. NDIO ANARUHUSIWA. [Any time he/she can allowed to Resign].

QUESTION NUMBER 7:

JE ni hatua zipi kwa kiongozi anapaswa kuzichukua akitaka kujiuzulu?

COUNTER:

Zimeelezwa vizuri katika Ibara ya 117(2) ya Katiba ya CUF;
1. kiongozi atajiuzulu kwa kuandika barua. Je Lipumba aliandika barua ya kujiuzulu? Jibu NDIO.

2. kuweka saini yake. Je Lipumba aliweka saini yake?. Jibu NDIO.

3. kuikabidhi barua hiyo kwa Katibu wa mamlaka iliyomchagua au kumteua. Je Lipumba aliikabidhi barua yake kwa Katibu wa mamlaka iliyomchaka? Jibu NDIO.

4. kiongozi huyo atahesabiwa kuwa amejiuzulu IKIFIKA TAREHE ALIYOAINISHA katika barua yake kuwa atajiuzulu. Je Tarehe aliyoianisha Lipumba kuwa atajiuzulu ILIFIKA? JIBU NDIO. aliainisha kuanzia Tarehe 5/8/2015 na kuutangazia umma kupitia vyombo vya habari kuwa amejiuzulu.

5. Pindipo akikubaliwa na mamlaka iliyomchagua au iliyomteua. Je Lipumba alitoa KUSUDIO LA KUJIUZULU NA KUHITAJI KUSUBIRI MAMLAKA ILIYOMCHAGUA KUMKUBALIA KUJIUZULU KWAKE? JIBU HAPANA. SHARTI LA KIKATIBA LIMEELEZA KUWA ATAHESABIKA KUWA [AMEJIUZULU [PAST] SIO ATAJIUZULU [FUTURE] ] IKIFIKA TAREHE ALIYOIAINISHA KATIKA BARUA YAKE KUWA KAJIUZULU. TAREHE ILIFIKA? NDIO NA SIO TU ILIFIKA BALI ILIKUWA NYUMA YA TAMKO LAKE ALILOLITOA RASMI PALE PEACOCK.

6. Kama hakuainisha Tarehe ya kujiuzulu kwake…? [THIS IS OPTION TWO AND MEANS THAT; NOT APPLICABLE IF OPTION ONE IS ALREADY FULLFILLED] Je Lipumba hakuainisha Tarehe ya kujiuzulu kwake? JIBU HAPANA. ameiainisha ilikuwa ni Tarehe 5/8/2015.

7. Basi atahesabiwa amejiuzulu mara baada ya Katibu wa mamlaka iliyomteua au kumchagua kupokea barua hiyo na mamlaka iliyomchagua au kumteua kukubali. [So long [a farewell remark] that Lipumba was Indicated the specific date of his RESIGNATION which is also defined as RETIREMENT, This condition was not Applicable again. Meanwhile The General Meeting was arranged and the matter presented for Discussion and Decisions]

Je Katibu wa Mamlaka iliyomchagua alipokea barua hiyo? JIBU NDIO.

Je Mamlaka iliyomchagua ilikubali kujiuzulu kwa Lipumba? JIBU NDIO. Katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza Tarehe 21/8/2016. Wajumbe 476 kati ya Wajumbe 700 waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Dharura wa Taifa walipiga kura ya KUKUBALI MAAMUZI YA LIPUMBA KUJIUZULU NAFASI YA UENYEKITI WA CHAMA TAIFA.

Hey Comeeee on!!!!!!!!!!!!!! Get-up, Stand-up.

ITAENDELEA SEHEMU YA PILI………………. [nimeiweka sehemu sehemu ili iwe nyepesi kueleweka na nisiwachoshe wasomaji]

CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.

HAKI SAWA KWA WOTE

Je, Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa na chuki binafsi dhidi ya Profesa Lipumba? III

Maharagande,
DECEMBER 28, 2017
 
haina haja ya sehemu ya pili....
nimeelewa vizuri kuwa lipumba hatakiwi kuwa pale buguruni kwa kikatiba ya cuf
 
Back
Top Bottom