Majibu kwa JK, Pinda na Mary Chitanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu kwa JK, Pinda na Mary Chitanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tzjamani, Mar 9, 2011.

 1. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Fr. Baptiste Mapunda - 2011-03-09 03:19 -- Mwananchi -> comments.
  Serikali ya CCM ijiulize kwa nini Chadema waandamane na kuwashawishi wananchi? Hili swali ni kubwa sana, si kwa suala la kuwang'oa wana CCm na seriali yao huo ni woga wa kunguru.
  Naye waziri Mkuu amekosea kabisa kusema kwamba" Rais ni mpole, mpole kwa nani, Rais anachagua ni mpole kwa Mafisadi wanaovuruga amani kwa njia ya kuiba mali ya umma. Lakini rais huyo siyo mpole kwa Wapinzani anaogopa nini? Inashangaza kiongizi wa ngazi ya juu kuogopa chama cha wapinzani ambao hawana jeshi la polisi, Jw, wala usalama wa taifa. Ila wao wana sera bwana zinazokubalika, wao wanatumia akili na kupanga mambo siyo kukurupuka tu kama wanavyofanya CCM ati kwa sababu ni watawala, hakuna kitu kama hicho, siasa zimegeuka wana CCM, jibuni hoja siyo jazba na vitisho vya nguvu ya dola.

  Mtamaliza risasi zote lakini watu watakuwepo tu, oneni yanayompakata Gaddafi si ya kurufrahisha, sasa miaka 41 anaharibikiwa kwanini hakuacha alipofika miaka 30 ya utawala wake? Shida kubwa ya viongozi wa Afrika ni kujiamini na "ULevi wa madarka". Mara nyingi naongelea ulevi wa pombe, madawa na ngono, lakini kwa CCM mmelewa madaraka, na hamuoni kama mnaweza kufanya makosa, sasa watu wengi wana macho mengi kuliko wewe mtu mmoja. Haya yote tunasema si kwa sababu tunaichukia CCM la hasha, mimi si mwanasiasa, nikipenda naweza kuwako kwani waliokuwako wana kitu gani cha pekee?

  Lakini kazi yangu kama kiongozi wa dini inanipa fursa ya kuiongoza, kuiasa, na kuikemea jamii, na wajibu huu sijapewa na serikali bali Mwenyezi Mungu. Hii ndiyo tofauti kati ya mbunge na mimi. Mimi sijachaguliwa kwa vidole na pengine wizi wa kura, la hasha. Kwa hivi ninyi mnaojisumbua kusema ati "tutoe majoho" kwa taarifa yenu hatutoa, na badala yake mimi nimeongeza majoho sita kwajili ya kuyatumia wakati nikiwa nahubiri habari njema ya wokovu si ya kifo wala ufisadi, wivu na chuki na uchochezi kama mnavyofikiria wengine na kuwapotosha wananchi juu ya viongozi wa dini na hasa kanisa katoliki. Daima nimesema na sasa mtasoma katika kitabu changu kipya "Unabii wa padre Mapunda jijini Dar es salaam Miaka 7' kwamba "Siasa bila dini ni wendawazimu". Tusijidanganye, ukisoma maandiko matakatifu utaona kwamba " Zamani manabii waliishi katika ikulu ya wafalme, lengo likiwa njia ya kuwaongoza, kuwakemea pale wanapopotoka na kuwashauri."

  Lakini leo hii viongozi wetu wa chama na serikali hawataki. Wao wameamua kuwa maadui wa madhehebu ya dini, na hili litawamaliza mpaka kiongozi wa mwisho. Kuwatukana na kuwakejeli viongozi wa dini ati kwa sababu wamekukosoa ni kosa kubwa sana. Inashangaza hata wale viongozi wa serikali na chama ambao wana imani na dini zao wameshindwa kuishauri serikali juu ya umuhimu wa dini katika taifa letu.

  Tutake tusitake, watanzania wengi wana dini zao, wewe unapowadharau, unazidi kujikaanga kwa mafuta yako, hii ni siri nawaambia viongozi wa serikali na chama. Wewe kumdharau kiongozi wa dini usijidanganye kwamba ndiyo umefika, kumbe umepotea. Hawa wananchi sisi tunakuwa nao saa mbili tu jumapili lakini hatuwaleti kwa magari, hatufanyi kampeni, wala kuwahonga unga, kanga, chumvi, vitambaa cha kichwani, pombe la hasha, bali wanafika wenyewe kwa hiari yao.

  Sasa pima hiyo, wewe unapowadanganya huko kwenye kampeni, ujue wanapohitaji amani, faraja, utulivu wanakimbilia kwa viongozi wa dini. kwa hivi ukisema kwamba sisi ni wadini huu ni uwongo mkavu na utawarudia nyie wenyewe. Kama kanisa katoliki lingependa kumpigia kampeni Dr. Slaa kwanza lingeshindwa? Lingeweza, kuna waumini wangapi katika idara mbali mbali, na mapadre wapo wangapi Tanzania na sisi tulio nje tupio wangapi, je tusingeweza mona hii ni kazi ya dakika tatu tu unamaliza ukiunganisha na elimu tuliyokuwa nayo ya kuwashawishi waumini hii mbona tunageuza nchi dakika tano tu.
  Kwa hivi mimi naonya msitu[NENO BAYA]ze kabisa, sisi ni waungwana tumeamua kufuata misingi ya demokrasia ya nchi yetu, kama kuna watu wanafanya kampeni basi ni swala la mtu binafsi lakini siyo msimamo wa kanisa. Na hivi propaganda za mwaka 1974 wala hazifai kabisa kwa sabau watz wamebadilika kabisa. Jamani tanzania ni yetu sote, hakuna sababu ya mtu au kiongozi kujifanya yeye anashika watu na ana watu, hata mimi nina watu je nani hana watu lakini shida ni kwamba unawatumia hawa watu kwa malengo gani? naomba sana viongozi wa chama na serikali wakati huu muangalie matamsi yenu, si kwa sababu ni viongozi mtaaminika la hasha. Tanzania ya leo n a sasa inahitaji kiberiti tu kuwasha moto katika nyasi kavu, kwa hivi wa kwanza ambao napenda wasikie ushauri wangu ni viongozi wa serikali na chama cha Mapinduzi, najua wengine mtasema Fr. mapunda anachuki binafsi, laini unajua moyo na mawazo yangu, hii ndiyo shida ya watanzania. Kuikosoa serikali siyo kuwa adui, lakini wengine tumezoea kusema ukweli, na ukweli unauma kweli kweli, lakini ndiyo dawa. Yesu alisema ' UKWELI UTAWAWEKA HURU" (John 8: 30). naona kule Mbinga- Ruvuma nyumbani kwetu wananchi bado wamelala usingizi tu, hawana habari wangoja kanga, pombne, vitambaa mwaka 2015, poleni sana amkeni ndugu, na wajibikeni kwa maendeleo yenu. Acheni tabia ya kusubiri serikali ndiyo kwa maana mnadanganywa kila miaka mitano. Wabunge wa Mbinga mpo? Msihofu na kufadhaika nikiuliza hivyo, ila watu wetu wanapigika kweli na uchakachuaji wa kura katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa halmshauri Mbinga ni kitendawili, je Mwenyekiti wa CCM ametoa jibu kwa wanaMbinga? Walikuwa wanamngojea huko mwezi desemba baada ya mwananchi mwenye mapenzi mema kupeleka ripoti kwa Mkurugenzi wa Takukuru, Rais na vyombo vingine, ningependa kusikia suala hilo limeshughulikiwa vipi? Jamani msishangae mtu kwao, mbona methali hii inafahamika sana, tunatka maendeleo ya bara bara Songea- Mbambayay, shule zenye walimu bora, kahawa yetu itusaidie inakufa, na maendeleo katika nyanja zingine. Watanzania amkeni usingizini. naipenda nchi yangu Tanzania ndiyo kwa maana inaniuma sana kuona inayumba.
   
Loading...