Maji: Tiba kubwa kuliko zote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maji: Tiba kubwa kuliko zote

Discussion in 'JF Doctor' started by Fatma Bawazir, May 2, 2011.

 1. Fatma Bawazir

  Fatma Bawazir JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  water.jpg

  5: Maji huzuia na kutibu ugonjwa wa kipandauso (migraines)
  Uumaji wa kichwa kwa mbele, ama kipandauso, huwa ni dalili ya ubongo na macho kuhitaji maji mwilini. Maumivu hayo yaweza kutoweka kabisa mara baada ya mwili kuwa na maji ya kutosha. Iwapo hali ya kuuma kwa macho na kichwa itaendelea kwa sababu ya upungufu wa maji, madhara yake ni kuvimba kwa macho na hatimaye kupoteza uwezo wa jicho kuona.

  6: Maji huzuia na kuponya uvimbe kwenye utumbo
  Maumivu ya tumbo yatokanayo na kuvimba kwa utumbo mpana, husababishwa na upungufu wa maji ambayo husababisha utumbo kujiminya ili kuokoteza maji yaliyosalia kwenye haja kubwa, na matokeo yake kumfanya mtu kutoa haja ngumu inayoambatana na maumivu makali.


  Baadaye hali hii ikiendelea, huweza kusababisha matatizo mengine makubwa, yakiwemo ya ukosefu wa choo kwa muda mrefu, kuvimba sehemu ya haja kubwa na kutokwa damu na hata kupatwa na saratani ya utumbo.

  7: maji na chumvi huweza kuzuia na kutibu pumu (Asthma)
  Ugonjwa wa pumu, ambao umeathiri mamilioni ya watoto duniani na kuua wengine wengi kila mwaka, ni matokeo ya matatizo mbalimbali yanayosababishwa na upungufu wa maji mwilini. Unywaji wa maji ya kutosha, hasa kwa kuchanganya na chumvi kidogo, hupunguza kasi ya mtu kushambuliwa na ugonjwa huo mara kwa mara.

  Bila kutambua kwamba chanzo cha ugonjwa wa pumu kwa watoto ni upungufu wa maji mwilini, mtoto akiendelea kwa muda mrefu kusumbuliwa na ugonjwa huo, vinasaba vingine vya mwili navyo huathirika na kufanya tatizo kuwa sugu na kuhatarisha uhai wa mgonjwa.

  8: Maji huweza kuzuia na kutibu shinikizo la damu
  Shinikizo la juu la damu (high blood pressure) linapotokea huwa ni matokeo ya jitihada za mwili kujaribu kuzoea ukame wa maji uliojitokeza kwenye mishipa ya damu ambayo hupeleka kwenye chembechembe hai za mwili. Unywaji wa maji yaliyochanganywa na chumvi kidogo huweza kushusha presha.

  Madhara yanayotokea baada ya mtu kutokujua tatizo lake limetokana na upungufu wa maji na akanywa dawa (diuretics) ambazo huchangia kukausha maji mwilini, husababisha kuziba kwa mishipa ya damu ya kwenye ubongo na hivyo mtu kupatwa na mshituko wa moyo na kupooza mwili. Vilevile tatizo hilo husababisha kuharibika kwa figo.

  9: Maji hutibu tatizo la lehemu mwilini (Cholesterol)
  Kuwepo kwa lehemu nyingi kwenye damu, huwa ni ishara ya matatizo katika mfumo wa uhifadhi maji mwilini. Hivyo unywaji wa maji ya kutosha kila siku, kutashusha kiwango cha lehemu na kunaweza kuondoa au kudhibiti tatizo hilo ambalo baadaye huweza kusababisha matatizo mengine.

  10: Maji huondoa mfadhaiko wa akili, tatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi, uchovu
  Tatizo la upungufu wa maji mwilini linapokuwa sugu (chronic), imeelezwa kuwa humsababishia mtu hata matatizo ya kufadhaika kiakili, kukosa hamu ya kufanya mapenzi na kujisikia mchovu wakati wote.

  Lakini utashangaa pale utakapoanza kunywa maji na mwili ukawa na maji ya kutosha, kwani matatizo yote hayo hutoweka. Kujiimarisha zaidi, utatakiwa kufanya na mazoezi ya viungo ili kurejesha mwili wako katika hali yake ya kawaida.
   
 2. n

  neyro JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 232
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  sanx kwa ku2kumbusha umuhimu wa maji. Wengine wamejisahau kabisaaa. Hebu tukumbushe 2nywe sio chini ya lita ngapi kwa cku?
   
 3. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  niliwahi kusoma mahala kuwa maji nayo yakiwa mengi mwilini husababisha madhara. naomba utudadalie pia
   
Loading...