MZK
JF-Expert Member
- Sep 13, 2012
- 240
- 309
PAMOJA na kupunguzwa kwa bajeti na idadi ya wanajeshi, Marekani imeendelea kuongoza kama nchi yenye jeshi lenye nguvu zaidi duniani, kulingana na ripoti juu ya utandawazi ya Credit Suisse.
Wakati Marekani ikiwa taifa kubwa kwa mbali kijeshi, Urusi na China zinaifuata kwa mbali. Canada, hata hivyo, ndiyo nchi dhaifu zaidi katika nchi 20 katika orodha hiyo.
Credit Suisse inasema kuwa upo ugumu wa kuwaza kupata nguvu halisi ya majeshi hayo kwa ajili ya kufanya ulinganifu. Ili kufanya hivyo, ripoti hiyo inatumia vigezo sita kwa ajili ya kujua nguvu halisi ya jeshi na kutoa maksi.
Vigezo vinavyotumiwa kwa ajili ya kupima nguvu ya jeshi na uzito wake kwa ujumla ni idadi ya wanajeshi (ambayo inatoa uzito kwa kiasi cha asilimia 5), vifaru (10%), ndege za kivita (20%), meli za kubeba ndege za kijeshi au aircraft carrier (25%), na manowari (25%).
Orodha hiyo inaelezea nguvu za kijeshi kwa maana ya kiasi na haiangalii ubora halisi wa silaha na mafunzo ya kijeshi ambayo majeshi hayo yanaweza kuwa nayo. Uwepo wa baadhi ya mataifa kwenye orodha kunaweza kuwashangaza baadhi ya watu.
Majeshi yenye nguvu zaidi duniani ni kama ifuatavyo:
20. Canada
Bajeti: $15.7 bilioni
Idadi ya askari: 92,000
Vifaru: 181
Ndege za kivita: 420
Manowari: 4
Canada ipo chini kabisa ya orodha sababu ya udogo wa jeshi lake, na kutokuwa na meli zinazobeba ndege na helikopta za kivita, na kwa kuwa na idadi ndogo ya vifaru na manowari. Lakini nchi hiyo imeshiriki katika operesheni za kijeshi huko Afghanistan na Iraki, na ni mwanachama wa NATO.
Canada pia ni menza wa Marekani katika mradi wa kuunda ndege za F-35.
Askari wa Canada akiwa kwenye doria huko Afghanistan.MCpl. Angela Abbey/Canadian Forces Combat Camera
No. 19. Indonesia
Bajeti: $6.9 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 476,000
Vifaru: 468
Ndege za kivita: 405
Manowari: 2
Jeshi la Indonesia limewekwa juu ya Canada kwa sababu ya idadi yake kubwa ya wanajeshi na idadi kubwa ya vifaru. Jeshi, hata hivyo, halina meli za kubeba ndege za kivita, na pia lina idadi ndogo za manowari.
No. 18. Ujerumani
Bajeti: $40.2 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 179,046
Vifaru: 408
Ndege za kivita: 663
Manowari: 4
Jeshi la Ujerumani lipo chini kwenye orodha kwa sababu ya haina meli ya kubeba ndege na ina idadi ndogo ya manowari, kitu ambacho, kulingana na njia inayotumiwa na Credit Suisse, inaipunguzia alama.
Hata hivyo Ujerumani ina idadi nzuri ya helikopta za kijeshi. Hivi karibuni, nchi hiyo imeanza kufikiria kutoa msaada wa kijeshi kwa mataifa ya Ulaya Mashariki ambayo ni wanachama wa NATO.
Vikosi maalumu vya Ujerumani.Fabian Bimmer/REUTERS
No. 17. Poland
Bajeti: $9.4 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 120,000
Vifaru: 1,009
Ndege za kivita: 467
Manowari: 5
Poland inaizidi Ujerumani kwa sababu ya idadi yake kubwa ya vifaru na idadi kubwa zaidi ya manowari. Nchi hiyo pia imezidisha matumizi ya kijeshi kutokana na vitendo vya Urusi huko Crimea na mgogoro unaoendelea huko Ukraine.
Wanajeshi wa Poland wakishiriki katika mazoezi ya kijeshi nje ya mji wa Yavoriv karibu na Lviv mwezi Septemba 19, 2014.Roman Baluk/Reuters
No. 16. Thailand
Bajeti: $5.39 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 306,000
Vifaru: 722
Ndege za kivita: 573
Manowari: 0
Jeshi la Thailand kwa sasa linaidhibiti nchi hiyo kufuatia jaribio la mapinduzi la Mei 2014. Jeshi hilo ni mhusika mkuu katika kuhakikisha umoja wa nchi hiyo. Nchi hiyo imepata alama kubwa kwa sababu ya idadi kubwa ya wanajeshi, idadi kubwa pia ya vifaru, na pia ina meli moja ya kubeba ndege za kivita.
Mwanajeshi wa Thailand akiwa kwenye doria kwa kutumia helikopta ya kijeshi baada ya kuwasili kusini mwa jimbo la Narathiwat Machi 2, 2007. Surapan Boonthanom/REUTERS
No. 15. Australia
Bajeti: $26.1 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 58,000
Vifaru: 59
Ndege za kivita: 408
Manowari: 6
Jeshi la Australia ni dogo – na ndiyo maana linapata alama ndogo katika eneo hilo na pia katika idadi ya vifaru. Pia ina idadi ndogo ya ndege za kivita.
Inapata nafasi nzuri kutokana na uwepo wa helikopta za kivita na manowari.
Askari wa Australia wa batalioni ya 5 wakati wa mazoezi ya kijeshi na jeshi la Marekani huko Hawaii nchini Marekani Julai 29, 2014.Hugh Gentry/REUTERS
No. 14. Israel
Bajeti: $17 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 160,000
Vifaru: 4,170
Ndege za kivita: 684
Manowari: 5
Kwa ujumla, Israel ina jeshi dogo. Lakini kutokana na mafunzo ya lazima ya kijeshi, idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo ni wanajeshi na wapo tayari kivita. Ikiwa na historia ya kuzungukwa na majirani wachokozi, Israel pia inaidadi kubwa ya vifaru, ndege za kivita, na helikopta za kivita.
Nchi hiyo pia ina ubora wa kijeshi. Ina jeshi zuri la anga, ndege za kisasa za kivita, ndege zenye teknolojia ya kisasa zisizotumia rubani, yaani drones, na silaha za kinyuklia.
Wanajeshi wa Israel katika mpaka wa nchi hiyo na Lebanon Januari 28, 2015.Ariel Schalit/AP
No. 13. Taiwan
Bajeti: $10.7 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 290,000
Vifaru: 2,005
Ndege za kivita: 804
Manowari: 4
Ikiwa inakabiliwa na tishio kutoka China, ambayo imeendelea kuwa na mipango ya namna ya kuvamia na kuichukua tena nchi hiyo, Taiwan imeelekeza nguvu zake katika kuendeleza jeshi lake. Kwa maana hiyo, kisiwa hicho ina inashika nafasi ya tano kwa kuwa na idadi kubwa ya helikopta za kivita. Pia ina idadi kubwa ya ndege za kivita na vifaru.
Mtu akiwa katika mafunzo ya kijeshi katika eneo lenye mawe katika pwani ya Taiwan kama sehemu ya mafunzo kwa jeshi la wanamaji wa nchi hiyo Januari 19, 2011. Hii ni sehemu ya mwisho ya mafunzo makali ya kipindi cha wiki 9. Nicky Loh/REUTERS
No. 12. Misri
Bajeti: $4.4 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 468,500
Vifaru: 4,624
Ndege za kivita: 1,107
Manowari: 4
Jeshi la Misri ni la zamani na kubwa zaidi katika Mashariki ya Kati. Linapokea msaada mkubwa kutoka kwa Marekani na linashika nafasi ya tano kwa idadi ya vifaru duniani. Lina zaidi vifaru 1,000 aina ya M1A1 Abrams kutoka Marekani.
Nchi hiyo pia ina idadi kubwa ya ndege za kivita.
Gari la deraya kwa ajili ya kubeba wanajeshi katika jeshi la Misri.Mohamed Abd El Ghany
No. 11. Pakistan
Bajeti: $7 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 617,000
Vifaru: 2,924
Ndege za kivita: 914
Manowari: 8
Jeshi la Pakistan ni mojawapo ya majeshi makubwa zaidi duniani, kwa maana ya idadi ya askari. Nchi hiyo pia inapata alama nzuri kutokana na kuwa na idadi kubwa ya vifaru, ndege za kivita, na helikopta za kijeshi.
Pia, nchi hiyo inadhaniwa kuwa inaunda silaha za kinyuklia kwa kasi kubwa kiasi kwamba itashika nafasi ya tatu kwa idadi ya silaha hizo katika kipindi cha miaka kumi ijayo.
Wanajeshi wa Pakistan wakisimamia wakati watu, ambao walikimbia operesheni ya kijeshi ya jeshi hilo huko jimbo la Waziristan, wakipewa misaada ya chakula huko Bannu.Thomson Reuters
No. 10. Uturuki
Bajeti: $18.2 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 410,500
Vifaru: 3,778
Ndege za kivita: 1,020
Manowari: 13
Jeshi la Uturuki ni mojawapo ya majeshi makubwa katika eneo la mashariki mwa bahari ya Mediteranian. Pamoja na kwamba haina meli ya kubeba ndege za kivita, ni mataifa matano tu katika ripoti ya Credit Suisse ndiyo yenye manowari nyingi zaidi ya Uturuki.
Pia, nchi hiyo ina idadi kubwa ya vifaru pamoja na ndege na helikopta za kivita.
Nchi hiyo pia ni mwanachama wa mpango wa ndege za kisasa kabisa za kivita za Marekani aina ya F-35.
Vifaru vya jeshi la Uturuki vikiwa katika mpaka wake na Syria karibu na mji wa kusini mashariki wa Suruc huko katika jimbo la Sanliurfa Oktoba 6, 2014.Umit Bektas/REUTERS
No. 9. Ungereza
Bajeti: $60.5 billion
Idadi ya wanajeshi: 146,980
Vifaru: 407
Ndege za kivita: 936
Manowari: 10
Pamoja na kwamba Uingereza inapanga kupunguza idadi ya wanajeshi wake kwa asilimia 20 kati ya mwaka 2010 na 2018, bado itakuwa na uwezo kutumia nguvu zake mahali popote duniani.
Jeshi la wanamaji la nchi hiyo, Royal Navy linapanga kuanza kutumia meli ya HMS Queen Elizabeth, kwa ajili ya kubeba ndege za kivita mwaka 2020, ikiwa na uwezo wa kubeba ndege 40 aina ya F-35B joint-strike fighter.
Koplo Birendra Limbu wa jeshi la Uingereza akiwaonyesha watoto wa Afghanistan bunduki yake wakati wakilinda eneo karibu na kizuizi cha polisi wa Afghanistan nchi ya mji wa Lashkar Gan katika jimbo la Helmand Julai 13, 2011.Shamil Zhumatov/REUTERS
No. 8. Italia
Bajeti: $34 billion
Idadi ya wanajeshi 320,000
Vifaru: 586
Ndege za kivita: 760
Manowari: 6
Jeshi la Italia limepata nafasi ya juu kwa sababu ya kuwa na meli mbili za kubeba ndege za kivita. Meli hizi pamoja na idadi kubwa ya manowari na helikopta za kivita, inaipa nchi hiyo alama za juu.
Ndege aina ya Eurofighter Typhoon ya jeshi la anga la Italia wakati wa operesheni ya NATO ya kulinda anga huko Zokniai karibu na Siauliai Februari 10, 2015.Ints Kalnins/REUTERS
No. 7. Korea Kusini
Bajeti: $62.3 bilioni
Wanajeshi: 624,465
Vifaru: 2,381
Ndege za kivita: 1,412
Manowari: 13
Korea Kusini imekuwa haina ujanja zaidi ya kuwa na jeshi kubwa lenye uwezo wa kukabiliana na uvamizi wowote kutoka Korea Kaskazini. Kutokana na hayo, Korea Kusini ina idadi kubwa ya manowari, helikopta za kivita, na wanajeshi.
Nchi hiyo pia ina vifaru vingi na jeshi la anga linaloshika nafasi ya sita kuwa ukubwa duniani kwa sasa.
Askari wa vikosi maalumu wa Korea Kusini wakishiriki katika mafunzo ya kijeshi.Cpl. Matthew J. Bragg/US Marine Corps
No. 6. Ufaransa
Bajeti: $62.3 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 202,761
Vifaru: 423
Ndege za kivita: 1,264
Manowari: 10
Jeshi la Ufaransa ni dogo, lakini askari wake wanamafunzo ya kutosha na lenye uwezo mkubwa.
Nchi hiyo ina meli mpya ya kubeba ndege za kivita Charles de Gaulle, na imekuwa inashiriki katika kupeleka askari wake katika nchi mbalimbali zenye migogoro barani Afrika na kupambana na ugaidi.
Askari waUfaransa wakiwa katika doria huko katika bonde la Terz, kiasi cha maili 37 kaskazini mwa mji wa Tessalit kaskazini mwa Mali Machi 20, 2013.Stringer ./REUTERS
No. 5. India
Bujeti: $50 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 1,325,000
Vifaru: 6,464
Idadi ya ndege za kivita: 1,905
Manowari: 15
India ni miongoni mwa mataifa yenye nguvu zaidi za kijeshi duniani. Ina idadi kubwa ya wanajeshi, inazidiwa na Marekani na China, ukiongeza na idadi kubwa ya vifaru, zaidi ya nchi yoyote kuacha Marekani, China au Urusi.
Nchi hiyo pia ina silaha za kinyuklia. Inatarajiwa kuwa nchi ya nne kwa matumizi makubwa zaidi ya kijeshi duniani ifikapo mwaka 2020.
Wanajeshi wa India katika kambi yao huko New Delhi Novemba 6, 2014.ovember 6, 2014.Adnan Abidi/Reuters
No. 4. Japan
Bajeti: $41.6 billion
Idadi ya wanajeshi: 247,173
Vifaru: 678
Ndege za kivita: 1,613
Manowari: 16
Kwa ujumla, jeshi la Japan ni dogo. Hata hivyo, nchi hiyo ina silaha za kutosha.
Kulingana na Credit Suisse, inashika nafasi ya nne kwa idadi kubwa ya manowari. Nchi hiyo ina meli nne za kubeba ndege za kivita, pamoja na kwamba meli hizi zinabeba helikopta za kivita tu.
Nchi hiyo inashika nafasi ya nne kwa idadi kubwa ya helikopta za kivita ikiwa nyuma ya China, Urusi na Marekani.
Vifaru na helikopta vikishiriki katika mazoezi ya kijeshi.Yuya Shino/REUTERS
No. 3. China
Bajeti: $216 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 2,333,000
Vifaru: 9,150
Ndege za kivita: 2,860
Manowari: 67
Jeshi la China limekua kwa haraka kwa maana ya ukubwa na uwezo katika kipindi cha miongo michache. Kwa maana ya idadi ya watu, ni jeshi kubwa kuliko yote duniani. Pia linashika nafasi ya pili kwa idadi ya vifaru, nyuma ya Urusi na pia inashika nafasi ya pili kwa manowari nyuma ya Marekani.
Nchi hiyo pia imefanya maendeleo makubwa katika miradi ya kulifanya jeshi lake kuwa la kisasa katika masuala mbalimbali ya teknolojia ya mapigano, ikiwemo katika makombora ya masafa marefu na kizazi cha tano cha ndege za kivita.
Askari wa China akishiriki katika mazoezi ya kijeshi wakati wa majira ya kipupwe huko Heihe, katika jimbo la Heilongjiang.REUTERS/CDIC
No. 2. Urusi
Bajeti: $84.5 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 766,055
Vifaru: 15,398
Ndege za kivita: 3,429
Manowari: 55
Jeshi la Urusi linashika nafasi ya pili kwa nguvu duniani. Nchi hiyo inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya vifaru, na inashika nafasi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya ndege za kivita nyuma ya Marekani, na pia inashika nafasi ya tatu kwa idadi ya manowari nyuma ya Marekani na China.
Matumizi ya kijeshi ya nchi hiyo yameongezeka kwa kiasi cha theluthi moja tangu mwaka 2008 na yanatazamiwa kuongezeka zaidi ya asilimia 44 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Nchi hiyo pia imeonyesha uwezo wa kutumia nguvu mbali na mipaka yake kwa kupeleka askari wake nchini Syria.
Askari wa Urusi wakiwa katika gari la deraya katika mji wa bandari wa Sevastopol huko Crimea Machi 10, 2014.REUTERS/Baz Ratner
No. 1. Marekani
Bajeti: $601 bilioni
Idadi ya wanajeshi: 1,400,000
Vifaru: 8,848
Ndege za kivita: 13,892
Manowari: 72
Pamoja na kupunguzwa kwa matumizi ya kijeshi, Marekani bado inatumia fedha zaidi – bilioni 601 – katika masuala ya ulinzi zaidi ya nchi nyingine zote 9 zinazoifuata kwa pamoja katika ripoti ya Credit Suisse.
Kitu ambacho nchi hiyo inazidi nyingine ni idadi kubwa ya meli za kubeba ndege za kivita, ambazo ni 10 na 3 zaidi zinatazamia kuingizwa katika matumizi ifikapo mwaka 2020. Ukiilinganisha na India, ambayo ndiyo kwanza inaunda meli yake ya tatu, ikiwa inashika nafasi ya pili kwa kuwa na meli za aina hiyo duniani.
Marekani, kwa mbali ina ndege nyingi za kivita kulinganisha na nchi yoyote duniani, teknolojia ya kisasa zaidi, jeshi kubwa na lenye mafunzo ya hali ya juu – na hiyo ukiachilia mbali silaha nyingi zaidi za kinyuklia duniani.