Majeruhi wa ajali Karatu wakiwa KIA tayari kuanza safari ya matibabu nchini Marekani

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Majeruhi wa ajali ya basi, Karatu wakiwa wanaombewa katika uwanja wa ndege wa KIA tayari kuanza safari ya kuelekea Marekani kwa matibabu.

tmp_10331-IMG_20170514_101842-1438281754.jpg

========UPDATES
Safari ya kwenda Marekani kwa matibabu wanafunzi watatu wa Shule ya Lucky Vicent imeanza muda huu baada ya kupandishwa kwenye ndege maalum ya shirika la Samaritan la Marekani na watatumia saa 20 kufika nchini humo.

Majeruhi hao ambao walikuwa wamelazwa hospitali ya Mount Meru ni Jofrey Tarimo, Doreen Mshana na Saida Awadh wameagwa leo jijini Arusha kwa ajili ya kwenda kwenye matibabu hayo wakiwa na wazazi wao na muuguzi mmoja.
Mwanafunzi wa Lucky Vicent akiagana na ndugu zake katika uwanja wa KIA, tayari kwa ajili ya safari ya Marekani kwa matibabu zaidi.
tmp_11880-IMG_20170514_123158-382548636.jpg

tmp_11880-IMG_20170514_121839376551508.jpg
tmp_11880-IMG_20170514_121851701803718.jpg
 
Hivi Serikali inajifunza nini hapo inapoona raia kutoka nchi nyingine wanachoma mafuta ya dege kubwa all the way hadi bongoland ili kuokoa maisha ya watu watu! Haipati fundisho lolote juu ya thamani ya uhai wa binadamu? Haiwezi kujifunza kuwa "humanity" ndio sifa kuu ya uumbwaji wa binadamu?
 
Back
Top Bottom