Katika hali isiyokuwa ya kawaida nchini Marekani. Jamii ya Kijasusi ya Marekani imeamua kumpa kwa vipimo ripoti za kijasusi Rais wa Marekani Donald Trump.
Habari zinasema kumekuwa na vita baridi kati ya Ikulu ya White house na jamii ya kijasusi ambayo Trump amekuwa akiilaumu hasa baada ya KUVUJA kwa maongezi ya Mteule wake na mshauri wake mkuu wa mambo ya usalama bwana Mike Flynn aliyelazimika kujiuzulu baada ya mazungumzo yake na balozi wa Urusi KUVUJWA hadharani.
Trump amekuwa akilaumu idara hizi kuwa ZINAVUNJA sheria kwa KUVUJISHA maksudi habari nyeti/classified za serikali kwa vyombo vya habari.
Pia jamii hii ya kijasusi imeanzisha uchunguzi dhidi ya baadhi ya wasaidizi wa Trump ambao nao huenda wamefanya ama wamekuwa wakifanya mawasiliano na maafisa wa Urusi.
Hili limemkasirisha Trump ni kama vile wanataka kumchafua ili aachie uongozi..
Nao maofisa wa kijasusi wanaogopa kumpa Trump SIRI ZOTE wakihofu tabia yake ya KUMSIFIA Vladimir Putin rais wa Urusi kama INAYOWAKERA.
Habari zinasema katika breafings ambazo hupewa rais kila siku WAMEZIPUNGUZA hasa zile zinazohusika na jasusi unaofanywa dhidi ya SERIKALI ZA KIGENI.
Kuna madai kuwa hawampi ushirikianao kama vile VYANZO ama NAMNA wanavyokusanya habari kutoka mataifa mbali mbali wanayoyafanyia ujasusi.
Moja ya wanabunge wa California aliyekatika kamati ya Bunge ya UJASUSI /Intelligence committee wa chama cha Democrat Adam Schiff amenakiliwa akisema kumekuwa na malalamiko ndani ya jamii hiyo.
Naye Trump amaeamua kwenda kwa wananchi ili awe karibu nao. Hivyo amaeamua kufanya mkutano wa hadhara katika mji wa Meliboun utakaohudhuriwa na watu walio na TIKETI maalum tu. Sijui kutoaminiana kati ya Trump na Jamii hiyo utafika wapi?
Chanzo: WALL STREET JOURNAL