Majaribio ya kupata leseni hakuna tena

Majaribio ya kupata leseni hakuna tena

Shida na raha

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
3,773
Reaction score
3,474
Kumekua na mtindo wa madereva kuendesha magari bila kujua sheria za barabarani na hili likiwa linachangiwa na leseni za vichochoroni.
Umakini hakuna katika ku-drive chombo, leo kuna ajali ilitaka kunitokea eneo la Mwembe ladu Zanzibar wakati nikiwa naendesha vespa nimetumia uzoefu wangu wa mda mrefu sikua kukwepa ajali hiyo.
Jinsi ilivyokua, jamaa alikua na gari mbele yangu Hendiketa amewasha ya kulia mimi nikaenda kushoto wakati huo huo ghafla nimekuta kapindisha kushoto mimi nilijua anapinda kulia kama hendiketa inavyoelekeza.
 
Kosa la 'hendiketa' sio la dereva. Dereva ye kaiambia hivi, yenyewe ikawaka hivi
 
Mimi nikajua ni madereva wa bodaboda tu ndio wenye huo wazimu............!!!!
 
Bodaboda wao hutumia indicator /hazard kama taa ya kuwasaidia kumulika kama taa haifany kazi, jichanganye ukutane nae road, utajuta
 
Pole sana.
Mie niliamua kama dereva anayekuja kawasha indiketa siingii mpaka aanze kukunja kona kwenda huo uelekeo. Madereva wengi huzisahau...
 
SHIDA NA RAHA sheria za usalama barabarani zinazohusu Madereva zote ni sawa,hivyo kupita ubavuni wa kushoto wa gari la mbele yako ni kosa ulistahili uwe nyuma ya gari la mbele yako.
 
Kuna hawa madreva wa gari za abiria utafikiri hawana akili wanalazimisha sehemu kupita hata kama hapana njia ya ku-overtake kisa wanakimbilia abiria sasa jichanganye ukutane nao hao nishida. Nimeshawakwepa sana maeneo ya round about wanaona huna thamani mwenye kuendesha chombo kidogo. Nimekumbuka kisa kimoja wakati gari ya abiria inataka ku-overtake mbele ikatoke gari nyingine kwa bahati mbaya ikaenda kugonga nyingine iliyokua kwenye site yake. Niwachekeshe sasa hiace iliyogongwa ikasimama wakati dereva na konda wanaenda kuomba msamaha wakakuta wajeda kama wa4 wamevaa kombati ndani ya gari hile ah! Walikula kona wakaacha abiria. Kumbe ile gari iliyogongwa inatumiwa na wajeda kwenda kazini.
 
SHIDA NA RAHA sheria za usalama barabarani zinazohusu Madereva zote ni sawa,hivyo kupita ubavuni wa kushoto wa gari la mbele yako ni kosa ulistahili uwe nyuma ya gari la mbele yako.

Mgosani mbona unaleta sheria mpya!!!? Indicator amewasha ya kulia ulitegemea nipite wapi.
 
Siku hizi majaribio yanafanyikia mifukoni...siku hizi hata vichaa wakiwa na hela wanapewa leseni.....
 
Siku hizi majaribio yanafanyikia mifukoni...siku hizi hata vichaa wakiwa na hela wanapewa leseni.....

Ni kweli unachokisema pesa ndo kila unaweza kumwona mtu ana leseni class karibia zote ila anachojua kuendesha ni automatic tu.
 
Majaribio zamani wakati wa Nyerere, hapo Myfair vishoka wamejaa kila corner,

Hao ma Trafic wetu ndiyo wauzaji wakubwa wa hizo leseni
 
Kuna umuhimu wa kuwapima akili wote waliopewa dhamana ya kutoa leseni, na baadae wapimwe akili wanaoomba leseni.

Utakuta dereva wa daladala au mara nyingine hata wa basi kubwa la mkoani anaendesha akiwa rafu rafu kuanzia mavazi hadi usafi wa mwili (hajachana nywele, hajapiga mswaki). Hizi ni dalili za awali kuwa huyu ni mtu wa hovyo, na bila shaka uhuni wake hautaishia kwenye kuvalia suruali matakoni, bali utaendelea hadi kwenye uendeshaji wake na matumizi mengine ya barabara...lkn utashangaa ana leseni Class C

Aliyemfundisha darasani, na aliyempa leseni wanafahamu kuwa dereva ni zaidi ya kunyonga usukani?
 
Back
Top Bottom