Majanga ya moto mbeya

ERIC JOSEPH

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
567
55
Tunahuzunika sana pia tunaumia na kunyanyasika kinafsi mana mpaka sasa hatima yetu tumekuwa kama watoto yatima mana hakuna msaada wowote tunaopata mana hata selikali inaongozwa na matamko huku zaidi utasikia tunafanya uchunguzi mwisho wa siku hatuludishiwi majibu kama kweli ni tatizo la TANESCO.

Tunaomba watulipe fidia mana nchi za wenzetu kabla ya kukata umeme huwa wanatoa talifa mfn nchin Zambia kama TANESCO kwao ZESCO hawajatoa taarifa wakiunguza vitu basi watawajibika kulipa. Lakini hapa kwetu watakujibu utumbo jiulize tokea uanze mgao watu wamepata hasala kiasi gani cha zaidi watakachokifanya wataingiza siasa, tungeomba kusema kuwa siasa zina mahala pake.

Roho inaniuma mana tokea moto ulivyotoke Mwanjelwa tulipoteza mali nyingi sana mpaka ndg zetu weng hata kimitaji tuliyumba sana tukauza mali zetu zilizokuwa zimebaki kwa kujikongoja. Kweli ng'ombe wa masikin hawezi kudumu tena leo tumepoteza hata kile kidogo sijui kesho itakuwaje.

Jaman umasikin mbaya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom