BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,126
By Muyonga Jumanne, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Changamoto ya ajira kwa madaktari ndiyo sababu ya jamii kukosa huduma muafaka kwa muda sahihi licha ya wahitimu wa fani hiyo kuwa wengi.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimwela amesema kati ya wanahitimu wa udaktari 2,000 kila mwaka, wanaoajiriwa na Serikali ni 400 pekee.
Dk Shimwela alikuwa anazungumza katika Siku ya Madaktari Duniani akibainisha kuwa wananchi wanakosa huduma kwa muda muafaka kutokana na upungufu mkubwa wa madaktari.
Amesema madaktari wasio na ajira wangeandaliwa mazingira mazuri ya kutoa huduma ya elimu juu ya uzazi wa mpango kwa wananchi, huku akitolea mfano Hospitali ya Amana ambayo watoto wanaozaliwa kwa siku ni 100.