Majambazi wavamia maduka na kuua mtu mmoja kwa kumpiga risasi mkoani Kagera

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Majambazi waliosadikiwa kuwa na Silaha za kivita, wanatafutwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera, kutokana na kuvamia maduka katika kijiji cha Nyakaiga wilayani Karagwe na kusababisha kifo cha mtu mmoja baada ya kupigwa risasi mgongoni.

Tukio hilo, lilitokea majira ya saa 2:30 jana (April 26) ambapo kundi hilo la majambazi lilivamia katika kijiji hicho na kuanza kufyatua risasi za hapa na pale hali iliyosababisha risasi moja kumpata mkazi mmoja kijiji hicho Ndyamukama Theonest(40)iliyompata sehemu ya mgongoni na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani hapa Augustine Ollomi, pamoja na majambazi hao kusababisha kifo na kuleta taharuki kwa wananchi katika kijiji hicho pia, wakifanikiwa kupora fedha kutoka kwenye maduka hayo ambazo hazijajulikana ni kiasi gani.

Ollomi alisema mara baada ya tukio hilo,majambazi hao walitokomea polini huku uchunguzi wa Jeshi la Polisi ulibaini maganda 21 ya risasi yaliyotumika na risasi 2 ambazo zilikuwa bado hazijakutumika hata hivyo uchunguzi wa kinterejensia unadhihihirisha kuwa kundi la majambazi hao,halikuwa la wenyeji wa eneo husika.
 
Kuongezeka kwa kambi za wakimbizi katika ukanda wa kagera, kigoma, utaathiri sana hali ya usalama. Maana hao wenzetu bunduki kwao ndy Visu.
 
Back
Top Bottom