Majambazi wanavamia maduka sasa hivi ninavyopost hapa Tabata Liwiti, nipo nawachungilia

Wanaume wa Dar wanaharibiwa sifa na watu kama wewe , ndo design ya hawa wanaochungulia majambazi na kuleta umbea huku basi bora urudi kwenu kilombero ijulikane.

Makaburi yamejaa majasiri, mashujaa na waliokuwa na roho za chuma.
Ujasiri bila nyenzo wala strategy madhubuti, ni sawasawa na ujinga. Kama huna silaha inayoeleweka huwezi kumparamia mtu mwenye bastola na bunduki, hata kama hana uwezo wa kuvitumia vyema, kwa sababu atakapobahatisha, uhai wako ndio utakaokuwa hatarini na hutakuwa na nafasi ya kuahirisha tukio. Kwa maana nyingine ni kuwa, akikupiga risasi kwa kubahatisha ukafa, hutafufuka tena ili ubadilishe kilichotokea.
 
Akawanyang'anye silaha?

Wengi wanaoshabikia kuwafuata hao majambazi, mlio wa risasi wanausikia kwenye movie.
Eti mtu ana silaha umparamie kishujaa wakati huna hata gobore? Yuko mbali na ulipo, huelewi wamejipanga vp. Majambazi unaowaona ni wale wenye jukumu la kuchukua fedha au chochote walichofata, mara nyingi huwa wanakuwa na mmoja mwenye silaha tena, alie na jukumu la kuwalinda na kuwashtua usalama wao unapokuwa mashakani na huwezi kujua alipokaa. Msidhani wote wanaouwawa kwenye matukio ya ujambazi ni wajinga.
 
Aliyekudanganya kwamba Policcm wanajali kiasi hicho ni nani? Nijuavyo mimi ni kwamba hata kama wakipigiwa sumu hawatakuja kwa wakati. Watasingizia ooh, Gari haina mafuta, Ooh tupo wachache kituoni na hatuwezi kufunga kituo tuje huko, Ooh hao majambazi wako wangapi na wana bunduki aina gani? Baada ya hapo watawasili kwenye eneo la tukio saa nne baada ya majambazi kuondoka. Polisi wa Tanzania ndio polisi ovyo kabisa duniani. Wewe ukitaka waje saa hiyo hiyo, wapigie uwaambie kuna wananchi wanafanya maandamano ya amani kudai haki zao za kiraia. Hapo ndipo utaona mikwara: Sio mabomu Ya machozi, maji ya kuwasha, risasi za mpira, na virungu, na baya zaidi, risasi za moto. Polisi bure kabisa hawana maana yeyote. Kutokuwapo kwao ni afadhali kuliko kuwapo kwao.

Teh teh teh!mkuu mbavu zangu mie duh!nimecheka saana, ase hivi ni kweli wanaweza kuuliza wezi wana bunduki aina gani! Ili iweje?, mkuu inamaana wanakuwa na maswali yote hayo, ase kama ni kweli basi hawawezi fika kwa wkt kwenye tukio.
 
We wa Dar pia?
No wonder hujui umuhimu wa filimbi!!! Mtaa wenu ukivamiwa mnaamshanaje kudhibiti hali?

Mkuu yaan kweli watu wa dar hadi leo mna amshana kwa filimbi yaan mambo ya miaka 47 still bado mnayatumia kwenye karne ya sayansi na teknologia?Halafu eti mna jiita mnakaa mjini???Mtaa wangu hatuwezi amshana kwa mafilimbi ili kama nyie.Sie tuna amshana kwa simu tu coz majirani wote tuna fahamiana.Ume sikia mvulana wa dar?
 
Dar ukipiga kelele za mwizi/wezi hakuna anayetoka sana sana kina kaka jambazi wakimaliza huko walipo wanakuja kwako uliyekuwa unawapigia kelele na lzm ukaonane na israel.
 
jamaa kasema anawachungulia dirishani na anaona mpaka silaha walizonazo we huoni umuhimu wa kuwapiga picha isaidie katika kuwakamata??angekuwa yupo mahala ambapo so Salama tusingeomba picha

Wewe hiyo ni hatari kwake ase, hata we nakushauri usije fanya kitu kama hicho, hivi unajua hata mtu mwenye elimu ya secondary tu anaweza kuisoma picha na kujua aliyepiga picha alikuwa wapi na kama ni mharifu anaweza kumfatilia na kumdhuru mda wowote au siku yoyote u never know, ni hatari na hasa kama unapiga toka ndani ya nyumba.
 
Mkuu yaan kweli watu wa dar hadi leo mna amshana kwa filimbi yaan mambo ya miaka 47 still bado mnayatumia kwenye karne ya sayansi na teknologia?Halafu eti mna jiita mnakaa mjini???Mtaa wangu hatuwezi amshana kwa mafilimbi ili kama nyie.Sie tuna amshana kwa simu tu coz majirani wote tuna fahamiana.Ume sikia mvulana wa dar?

Rudia kusoma ulichoandika kuhusu mnavyoamshana wakati mmevamiwa halafu utafakari upya huo mkakati wenu. Msilete ubishoo kwenye suala la ulinzi nyie watu.

Wazia muda wa simu kuunganishwa hadi mtaa wote muwasiliane, halafu ukiwa unavamiwa unapigaje simu? Filimbi ni chap. Na inampagawisha jambazi/mwizi asijue wapi salama.

Hebu fikiria mtaa wenye nyumba km 30 wote wapige filimbi.... manake hao majambazi hawana pa kwenda coz hiyo kelele tu wenge la hatari. Na mtaa wa jirani pia wanastuka so nguvu kubwa. Kwenye ulinzi, kuna teknolojia/zana bado ni mujarabu sana.

Btw... mi si mkaazi wa dar. Na uvulana nimeupita kitambo sana ndo maana sijihusishi na kebehi na ngebe kama wewe!
 
tofautisha kati ya wezi na majambazi!

Hao wanaopora madukani mithiri ya PANYAROAD ni wezi lakini majambazi ni wakina:- Chenge, Mramba ,Ngeleja , Tibaijuka , Mwambalaswa, na genge lote la magamba akiwemo jangili Lukuvi!!
 
hivi ninavyoongea muda huu majambaz wanapora pesa hapa tabata liwiti kwenye duka la jiran yetu bwana mganga,nipo dirishan nawaangalia wapo kama wanne mmoja akiwa na bunduki na bostola, dah hapa tumekusanyika watu mpaka sasa polis hawajafik,muuzaji kazilai,ntatuma picha soon za tukio.

Ungepiga simu polisi ndyo uje kupost hapa.
 
Ndio maana majambazi yanatamba.....miaka ya themanini wanafunzi wa shule ya msingi waliwahi kusaidiana na askari mmoja wa CID kudhibiti majambazi wenye silaha huku wanafunzi wakitumia mawe.......hii ilitokea Mwanza kipindi hicho...

Hai ndiyo wanaume. Siyo mwanaume unaona matukio kama hayo unakimbilia ku post. Wanaume dar vipi nyie?
 
Apigie jirani zake wapige filimbi wote kwa pamoja halafu jamaa wakipagawa wawatokee kwa umoja. Wanaume mkiwa na adui mkubwa mnaunga nguvu. Sio kuposti JF. Upuuzi huu...

Eti filimbi halafu watoke nje.
Umtokee jambazi mikono mitupu? Au huwa hamuoni mauaji ambayo majambazi wanaacha nyuma?
Ambacho kingesaidia ni majirani kupiga simu polisi then kuwasiliana wao kwa wao. Wenye bastola hata mmoja akirusha risasi hewani ndio zifuate hizo kelele hapo rahisi hata kuwatokea na watakimbia tu.
Japo umakini unatakiwa.
Halafu mkue bunduki sio panga maana mnaona rahisi tu.
 
Back
Top Bottom