MAJAMBAZI wenye silaha zinazodhaniwa kuwa za kivita wamevamia Kituo Kikuu cha Wilaya ya Kipolisi ya Nyamwaga na kumimina risasi za moto katika ofisi zake na makazi ya maofisa wa polisi wanaoishi karibu na ofisi hizo.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi Tarime, Constantine Masawe, amesema majambazi hao walivamia nyumba tatu tofauti zilizopo meta 20 kutoka kituo cha Polisi juzi saa tano usiku na kuwaweka watu chini ya ulinzi na kisha kuiba idadi kubwa ya ngombe na mbuzi wa eneo hilo.
Akiwafariji wananchi wa kijiji cha Nyamwaga jana asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Frank Uhalula ambaye aliitisha mkutano wa hadhara wa dharura, alisema ni jambo la kumshukuru Mungu kwamba hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo kwa sababu risasi hazina macho.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa dharura, baadhi ya wananchi waliomba serikali kutafuta mbinu mbadala ya kukabiliana na wimbi la uhalifu katika Wilaya ya Tarime.
Baadhi ya wanakijiji hao walimwambia Uhahula kuwa polisi waliopo katika eneo hilo wana umri mdogo na hawana uwezo wa kubeba silaha nzito na kupambana na majambazi.
Hao askari waliopo hapa ni watoto wadogo. Tunaomba askari waliokomaa na wenye uzoefu kupambana na majambazi, alisema mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Francis Ghati.
Wengine waliomba serikali ipeleke Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika wilaya hiyo na kutangaza hali ya hatari katika eneo hilo.
Tunaomba hata wanajeshi wastaafu wapewe bunduki watusaidie, Mathias Juvinali ambaye ni mwanajeshi mstaafu alisema.
Mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Wankio Wambura alisema: Huu ni ujumbe kwa Kanda Maalum ya Kipolisi Serikali inapaswa kuweka kambi ya kijeshi hata Tarime kwa sababu inaonekana polisi wameshindwa."
Akijibu hoja hizo, Uhahula alikiri kuwa kuna haja ya vyombo vya dola kujipanga upya kukabiliana na hali hiyo. Hili sio jambo jepesi. Ni kituo cha polisi kilivamiwa na polisi wetu hawakutoka hata kujibu. Ushauri wenu nimeuchukua na nitamwambia IGP, alisema Uhahula.
Hadi jana polisi walikuwa katika msako wa kutafuta mifugo iliyoibwa bila mafanikio.
Kifaa cha mawasiliano ya kipolisi (radio call) kiliokotwa na wananchi na kurudishwa Polisi huku kikidaiwa kuwa mmoja wa polisi hao alikidondosha alipokuwa akikimbia.
Tukio hilo la kuteka kituo cha polisi na kuiba mifugo limetokea ikiwa ni chini ya mwezi mmoja tangu watu wasiojulikana walipovamia familia tatu za ukoo mmoja na kuua watu 17 na siku chache baadaye kuvamia harusi na kuua watu watano kwa risasi.