Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,229
- 23,916
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa, Kassim Majaliwa
amewataka Makatibu Tawala wa
Mikoa nchini kuchukua hatua kali
kwa wote waliosababisha kuwepo
kwa watumishi hewa.
Amesema suala hilo la watumishi
hewa limeisababishia serikali
hasara kubwa hivyo ni lazima
watu wote waliohusika katika
mchakato huo wabainishwe na
wachukuliwe hatua kwa mujibu wa
sheria za utumishi.
Waziri Mkuu,Majaliwa ameyasema
hayo leo (10 Aprili,2016)
,alipokuwa akipokea taarifa ya
maendeleo ya mkoa wa Lindi
iliyowasilisha na mkuu wa mkoa
huo, Godfrey Zambi katika siku ya
kwanza ya ziara yake ya kikazi
wilayani Ruangwa .
Baada ya kufanyika kwa zoezi hilo
jumla ya watumishi hewa 7,795
walibainika ambao
wameisababishia serikali hasara
ya sh. bilioni 7.5.
Waziri Mkuu amesema zoezi la
kubaini watumishi hewa linalenga
kuokoa fedha za serikali ambazo
zilikuwa zinalipwa watumishi
waliokufa, kustaafu wengine ni
wale ambao wahusika walijiwekea
majina na kisha fedha kuingia
mifukoni mwa wajanja.
Awali Mkuu wa mkoa wa
Lindi,Godfrey Zambi katika taarifa
yake kwa Waziri Mkuu amesema
mkoa huo una jumla ya
wafanyakazi watoro 57 na hewa
saba ambao ni
marehemu,wastaafu waliokuwa
wanalipwa mishahara na
kuisababishia serikali hasara ya
sh. milioni 36 kwa mwezi mmoja.
Amesema zoezi hilo la kubaini
watumishi hewa na watoro
litakuwa endelevu na
wameanzisha timu kwa ajili ya
kufanya uchunguzi ili kubaini
sababu zilizosababisha watumishi
waliokufa au kustaafu kuendelea
kulipwa.