mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,310
- 6,544
Waziri Mkuu ameyasema hayo katika Kongamano la Mmomonyoko wa Maadili na vita dhidi ya Dawa za Kulevya lilioandaliwa na BAKWATA.
Maneno ya Waziri Mkuu:
"Serikali imepanga kushughulikia mtandao wote wa uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya.
Tumeunda tume ya kupokea taarifa, kuchunguza na hatimaye kushtaki. Tusitumie nafasi hii kushitaki kwa chuki tu, hii haitokuwa na nafasi.
Tume hii itapokea taarifa na kuchunguza, kama hana hatia tutamuacha na wala hatumtangazi. Tukigundua jambo hilo lipo, tutachukua hatua.
Tuna Kamishna wa uchunguzi, Kamishana wa kukamata, mwanasheria, Mkemia. Kwa walioathirika kuna daktari, Serikali imejipanga kweli kweli.
Katika kukamata hatutajali heshima, wadhifa wala kujulikana kwa mtu tukigundua anazalisha, anasafirisha, anauza au kutumia.
Baraza liko tayari na limeanza kazi, tumepata watu wengi na tunaondoka nao kweli. Msione kimya sisi hatutangazi mtu, hatutaki umaarufu tunataka tuone watu wanachukuliwa. Tunataka tupate mzizi mpaka jani.
Takwimu zinaonesha tuna vijana wasiopungua 1090 ktk magereza mbalimbali duniani. Wengine wanatumia 'patex' ya kuzibia viraka vya mabaskeli. Patex haipatikani madukani kumbe nayo ni 'dude', vijana wananusa na kulewa.
Pia tunaangalia aina ya madawa maabara na mahospitalini kuwa yanatengeneza kitu kingine. Tusijikite tu kwenye cocaine na heroin, kuna dawa nyingine za matumizi mengine kabisa zinatumika vibaya.
Sasa hivi tumepata mitambo ya hatari, usikubali kubeba mzigo bila kujua ndani kuna nini. Ukibeba mzigo ukitupitia jirani tutakujua. Hata ukiwa nyumbani kwako tukipita nje itatuonesha kuwa nyumba hii kuna mzigo, tutarudi reverse.
Hata ukiwa katikati ya kundi kuna chombo kitatuleta hapohapo ulipo, kitatuonesha ni huyu ana mzigo. Usikubali kubebeshwa mzigo usiojua ndani una nini, utapewa 'zigo' tukikukamata tutajua ni wako. Muwe makini.
Hivi sasa watumiaji wameenda mpaka vijijini. Ni jukumu la viongozi wa serikali ktk ngazi zote kujenga mifumo inayotupa taarifa ya nani anahusika na janga hili.
Matumizi ya dawa hizi yanakwenda sambamba na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI. Hii inachangiwa na kushirikiana sindano, kujiuza ili kupata pesa ya kununua 'unga' na namna nyingine nyingi.
Mateja wanahangaika kupata dawa za kulevya, hazipatikani kwa urahisi. Wengi tumeanza kuwaona kwenye hospitali zetu. Tunataka kufanya mabadiliko makubwa. Kuanzia Januari 2015 hadi Desemba 2016, Kilo 77 za heroin, 32.3 za cocaine zimeweza kukamatwa. Jumla ya Kilo 78,656.179 za bangi pia zilikamatwa na Ekari 71 za mashamba ya bangi ziliteketezwa."