DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Kyara, ameahidi kushughulikia kwa haraka changamoto ya msongamano wa magari katika jiji la Dodoma, akisema tatizo hilo limekuwa likitesa wakazi wa majiji makubwa nchini na kudhoofisha shughuli za kiuchumi na kijamii.
Akizungumza na wakazi wa Kata ya Majengo jijini Dodoma katika muendelezo wa kampeni zake, Kyara amesema serikali yake itajikita katika kuboresha miundombinu ya usafiri na kupanga upya mfumo wa usafirishaji ili kuhakikisha foleni zinapungua na wananchi wanapata huduma kwa wakati.
Mbali na hilo, Kyara ameahidi kurejesha dhana ya uadilifu na uaminifu katika utendaji wa serikali, akisema ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa. Alieleza kuwa serikali yake itajenga misingi ya utawala bora kwa kuzingatia maadili yaliyowekwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kyara aliambatana na mgombea mwenza wa nafasi ya urais, Satia Mussa Bebwa, ambapo kwa pamoja waliwaomba wananchi kuwapa ridhaa ya kushika dola ili kutekeleza vipaumbele vyao vikuu ambavyo ni: Kilimo chenye tija, Afya bora kwa wote, na Ajira kwa vijana.

.