goldie ink
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 5,636
- 9,132
Habari za wikiendi mabibi na mabwana,
Naamini mnaendelea vizuri na Mungu anawalinda katika kila jambo jema mnalolifanya, pia harakati za maisha yetu naamini pia bado tunaendelea kupambana kwa namna Moja au nyingine.
Nimeona leo sote kwa pamoja kama wanachama wa jamiiforums tuweze kujadiliana kwa mapana kuhusu kupata fursa za kibiashara / uchumi ili kuweza kuendelea kujikimu kimaisha bila kujali changamoto gani itatokea,
Ni vyema pia ningependa kuanza kueleza kwa kina kuhusu fursa hizi ili tuweze kupata urahisi wa kufafanua / kujadiliana kuhusu mada hii husika.
Ninaposema fursa za kibiashara nilikuwa na maana ya kwamba ni biashara gani ambayo tunaweza kuifanya na maeneo gani ambapo pamefulia kwa shughuli za kibiashara, uhitaji mkubwa / mdogo wa bidhaa kwa watu wake, soko lake pia limekaaje.
Mimi kama kijana nimeona bora nije huku ili niweze kupata mawazo mbali mbali kupitia nyinyi na mimi pia nitatoa mawazo yangu ila kuna wengine pia wananufaika na mjadala huu husika.
* Kwanza nilifikiria kufanya biashara ya chakula kwa mkoa wa mbeya, na mwanza,
* biashara ya kufuga kuku wa nyama na mayai katika mkoa wa dar es salaam.
* kufanya biashara ya kubuni mitindo mbali mbali ya nguo kwa mfumo wa kupiga chapa na kuprinti,
* kutengeneza sigara kwa kutumia tumbaku ya daraja la kwanza, na kufanya sigara kuwa na muonekano mzuri, na yenye ubora.
Mwenye wazo lingine ambalo anaona ni fursa nzuri ya kiuchumi ambayo tunaweza kuifanya iwe dar es salaam au mikoani, changamoto za hiyo biashara.
Ahsanteni sana ndugu zangu wa JF, karibuni pia kwenye haya majadiliano.