Maiti ya mwisho mauaji Arusha yapelekwa Kenya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maiti ya mwisho mauaji Arusha yapelekwa Kenya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwili wa marehemu Paul Njuguna Kaiyehe (26), raia wa Kenya ambaye aliuawa na polisi kwa risasi wakati wa maandamano ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Arusha Januari 5, mwaka huu, ulisafirishwa jana na unatarajiwa kuzikwa leo.
  Mwili huo ulisafirishwa kutoka Arusha kwenda Nakuru, Kenya kwa ajili ya mazishi.
  Mapema jana, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), alimkabidhi Balozi Mdogo wa Kenya nchini, Robert Mathenge, Sh. milioni mbili kwa ajili ya kusaidia kusafirisha mwili wa marehemu Kaiyehe.
  Akitoa rambi rambi hiyo, Lema alisema: “Mnajua ndugu zangu nawapa pole sana, huu msiba umetufika wote, baada ya ndugu yetu kupigwa risasi eneo la Jogoo House, akiwa katika shughuli zake na siyo kama alikuwa katika maandamano ya Chadema.”
  Aidha Lema alisema marehemu huyo alipigwa risasi umbali wa kilomita moja toka kituo cha polisi na hiyo inaonyesha kuwa polisi walivyokuwa wakipita mitaani na kuua watu ovyo.
  Lema alisema cha kusikitisha ni pale polisi, walipomjeruhi na kumuacha marehemu kwa saa tatu na kisha kumchukua hadi hospitalini na kufariki kutokana na kucheleweshewa huduma.
  Hata hivyo, aliomba msamaha kwa Kenya kwa yaliyotokea ili kudumisha ushirikiano kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Baada ya Mathenge kupokea rambirambi hiyo, alimkabidhi kaka wa marehemu, Timothy Gitau Kaiyehe, ambaye alimshukuru Lema kwa kuwasaidia kuwawezesha kupeleka mwili wa ndugu yao kwao ili wakauzike.
  Maandamano ya Chadema Mara yaahirishwa Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi mkoa wa Mara limesema hakutakuwa na maandamano yaliyokuwa yametangazwa na Chadema mkoa wa Mara ambayo yangefanyika leo.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Robert Boaz, alisema amefanya mazungumzo na Katibu wa Chadema mkoa wa Mara na kumhakikishia kuahirishwa kwa maandamano hayo.
  “Nimezungumza na katibu wa Chadema mkoa, mwenyewe kaniambia hakuna cha maandamano kwa kesho (leo). Hata hivyo, walikuwa hawajatuharifu kuhusu maandamano hayo licha ya kuzungumza na vyombo vya habari,” alisema Boaz.
  Chadema mkoa wa Mara kilitangaza kuitisha maandamano makubwa kwa ajili ya kupinga kile walichokiita vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji haki za raia vilivyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha.
  Katibu wa Chadema mkoa wa Mara, Nyanza Sibitali, aliliambia NIPASHE juzi kuwa maandamano hayo yalitarajiwa kufanyika leo na kuhusisha majimbo saba ya uchaguzi ya mkoa wa Mara na kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara kupeleka ujumbe huo.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...