Maisha yanazidi kuwa magumu, familia inanitegemea na sinachochote cha kuwapa. Kichwa kinawaka moto sijui la kufanya!

Ukosefu wa ajira hapa Bongo ni kama wimbo wa Taifa kila mtu anaweza kuimba, usikate tamaa, Omba Mungu kwa imani milango yako ya baraka itafunguka.
 
Binafs mambo yamenizidia kuwa magum sana, niseme nimefilisika, nimekubaliana na hali, sina ajira tena, sina pesa tena sijui nianzie wapi, huku nyuma familia inanitegemea, mke na mtoto mmoja wanahitaj huduma.

Nahisi kuchanganyikiwa muda mwingine unatembea kama kichaa, huku unawaza. Yaani natamani kwenda kutafuta maisha sehem yoyote yenye fursa lakini najiuliza nitaenda wap, na Dar bila kujishughulisha ni pagumu sana.

Mwenye ushauri au msaada wowote ule wa kazi tafadhal anaweza nisaidia, kwa maana akili yangu kiukweli ime-stuck, kichwa nahisi cha moto sana, kishakuwa kizito.

Eeeh Mungu wangu nishike mkono.
Mke wako anafanya kazi gani?
Kama hana kazi. Afanye biashara hata ya kutembeza mboga za majani na matunda mtaani.
 
Ukosefu wa ajira hapa Bongo ni kama wimbo wa Taifa kila mtu anaweza kuimba, usikate tamaa, Omba Mungu kwa imani milango yako ya baraka itafunguka.
Hivi kidume ameshindwa hata kwenda kuchoma mkaa Msata? Vipi huyo mwanamke ameshindwa hata kwenda kusafisha sahani na mabakuli kule kwa mamalishe? Hizo Mb anazotumia kuandika humu Jf anazipataje kwa mfano.
 
Kichwa iko waka moto, my friend you are not alone
images - 2023-12-26T162513.717.jpeg
 
Suluhu ya Kupata pesa na kuepuka kufilisika ni kulipa ZAKA baas.

Anza nw,

Chukua Kiasi chote ulichonacho saiz mfukoni, kiasi ambacho ndo pekee ulichonacho,

Kichukue ukawape maskini zaidi,

Au mpelekee mtumishi wa Mungu akuombee,

Mungu ameruhusu tumjaribu Kwa matoleo na ZAKA.

Usipuuzie nlokwambia. Utafunguliwa kipato chako, utapata deals na hutoamini,

Na kuanzia Leo, badilika, Kila ukipatacho, Tenga 1/10, hiyo ni ZAKA.

Ni hayo tu.
"au mpelekee mtumishi wa mungu akuombee" acha ujinga ww hela hana watoto na mkewe hawajala hiyo zaka anaitoa wp? ninyi watumishi mbuzi ni watu wa hovyo hovyo tu shuwain!
 
"au mpelekee mtumishi wa mungu akuombee" acha ujinga ww hela hana watoto na mkewe hawajala hiyo zaka anaitoa wp? ninyi watumishi mbuzi ni watu wa hovyo hovyo tu shuwain!
Kwani kichwani mwako huna ushauri Hadi uboreshe ushauri walotoa wengine?
 
Mnao ongelea kanisani .Hivi msha wahi kwenda kanisani una shida ata ya kodi au msaada wowote uka pewa ?? Amna sehemu ngumu kupata msaada wa pesa kama kanisani
 
we jamaa una makosa ya kisarufi na uandishi ila una contents balaa

Bado unao muda mwingi sana wa kujipanga. Wewe ni Me (na ujitambue hivyo). Kazi za kufanya ili uendelee kuishi ni nyingi sana kama wadau walivyobainisha huko juu. Cha msingi ni usichague kazi (kazi halali) na usiionee aibu kazi fulani. Kumbuka cheti chako cha Uhandisi ni karatasi tuu linaloweza kutumika ikitokea fursa, lakini ukifanya kazi nyingine yoyote inawezekana. e.g. sasa hivi Upo ujenzi wa majumba unaoendelea kila leo katika miji yote mikubwa na midogo hapa Tz. Ukienda huko kutafuta kazi ya saidia fundi unapata bila masharti yoyote - alimradi uwe tayari unaweza na ukubali malipo ya kati ya Tzs elfu 10 - 15 kwa siku.
Tena huku kwetu Umasaini ndani-ndani huku, wapo vijana wanasambaza maji dumu 1 (lts 20)kwa Tzs 300 - 500. Kitoroli au kiberenge kina uwezo wa kubeba madumu 6 -10 kwa mara moja. ref. Mtaji wa maskini ni nguvu zake.
BTW: Kazi zipo ila Watu / Vijana kama ww wanazionea haya eti nitajidhalilisha. Wengine hawataki kuondoka/ kutoka kwenda kusaka fursa kwingine e.g. hapo Dar. utadhani vijana wa hapo wamelogelezewa kukaa Dsm. tu kana kwamba ni marufuku kuondoka hapo.
Wa

Wanasema kijana ili utajirike ni lazima uishi Dar, kwamba ukiishi nje ya Dar sahau kuhusu utajiri japo mleta mada anaishi Dar na maisha yamemchapa, sijui ukweli ni upi.
 
Binafs mambo yamenizidia kuwa magum sana, niseme nimefilisika, nimekubaliana na hali, sina ajira tena, sina pesa tena sijui nianzie wapi, huku nyuma familia inanitegemea, mke na mtoto mmoja wanahitaj huduma.

Nahisi kuchanganyikiwa muda mwingine unatembea kama kichaa, huku unawaza. Yaani natamani kwenda kutafuta maisha sehem yoyote yenye fursa lakini najiuliza nitaenda wap, na Dar bila kujishughulisha ni pagumu sana.

Mwenye ushauri au msaada wowote ule wa kazi tafadhal anaweza nisaidia, kwa maana akili yangu kiukweli ime-stuck, kichwa nahisi cha moto sana, kishakuwa kizito.

Eeeh Mungu wangu nishike mkono.
Jichanganye uanze kupiga kazi ndogo deiwaka za ujenzi na kubeba mizigo ya wateja Cha kufanya amka mepema kaa kwenye Hardware wanalouza vifaa vya ujenzi mpaka jioni haukosi buku ten au buku saba za kununulia dogo na dagaa
 
Binafs mambo yamenizidia kuwa magum sana, niseme nimefilisika, nimekubaliana na hali, sina ajira tena, sina pesa tena sijui nianzie wapi, huku nyuma familia inanitegemea, mke na mtoto mmoja wanahitaj huduma.

Nahisi kuchanganyikiwa muda mwingine unatembea kama kichaa, huku unawaza. Yaani natamani kwenda kutafuta maisha sehem yoyote yenye fursa lakini najiuliza nitaenda wap, na Dar bila kujishughulisha ni pagumu sana.

Mwenye ushauri au msaada wowote ule wa kazi tafadhal anaweza nisaidia, kwa maana akili yangu kiukweli ime-stuck, kichwa nahisi cha moto sana, kishakuwa kizito.

Eeeh Mungu wangu nishike mkono.
Khaaa nilishapitiaga hio hali

Jikaze,pambana, Fanya kazi yoyote halali inayokuingizia kipato,usione aibu
 
Niliwahi kupitia kipindi kama hicho mwaka 20007 nilikuja Dar es Salaam nikiwa na pesa kiasi cha 13m ila zile pesa zote ziliyeyuka nikaanza kudaiwa kodi ya nyumba pale Shekh lango nikaona nimwambie mke nilie kuwa arudi kwanza kwao mimi nikakimbilia Tabora nako maisha yalikuwa Magumu zaidi baada ya mwaka mmoja nikabahatika kupata lifti ya roli mpaka Chalinze kisha nikarejea tena Dar nikafikia kwa dada yangu japo maisha pale kwa dada yalikuwa mazuri sana moyoni nilitamani kuwa mmiliki wa pesa zangu hata kama zingekuwa ndogo bado zingeweza kunitoa katika unyonge
Nilianza kutoka alfajiri nakutembea pembezoni mwa jiji la Dar nikisaka vibarua vya ujenz. Siku yakwanza nilianza kwa kubeba tofari niliuziwa tofari 600 kila tofari jamaa alikuwa analipa 50 kiukweli niliona hiyo kazi kama ni ukombozi nilivua nguo zangu za kistaaf nikabaki na pensi huku nikiwa kifua wazi nikaanza kukimbiza kiukweli haikuwa rahisi ukizingatia ndio ilikuwa mala yangu yakwanza kufanya mishe ya namna hiyo lakini kila nilipo tua tofari niliuapiza moyo wangu nakuambia hakuna kukata tamaa

Jua lilianza kuzama nikiangalia zile tofari zilikuwa bado nyingi nikamfata yule bosi ili aniruhusu nisombe mpaka usiku yeye aliniambia anaho hitaji ni tofari kufika site

Mwanga wa mbalamwezi na upepo utokao kwenye fukwe za kunduchi kiujumla vilinipa faraja nakuujaza moyo wangu hisia za ushindi kwa hakika tofari zilikuwa zikipungua ungedhani nilitumia fork lift ilipo fika saa saba usiku tayari nilikuwa nimehitimisha kuzibeba tofari 600 bosi alikuwa amenipa Advance ya 5000 ilio nifaa kwa maji na chakula

Asbuhi alipokuja alibaki kinywa wazi toka siku hiyo alinipa uongozi wakusimamia site yake nilifanya kazi kwa uaminifu mkubwa na hatimae nikawa napewa kazi na marafiki wa yule bosi maisha yangu yalianza kurudi nakusahau zile milioni 13

Nikafungua ukurasa mpya wa maisha nikasahau vyote nilivyo wahi kuvimiliki hapo Awali nikawa na malafiki wapya wenye kipato cha chini wakanionyesha vyumba vya bei rahisi nikaanza upya maisha japo sikuweza kurudiana na yule mke wa Shekilango lakini maisha yangu yalikuwa ni maisha yenye Furaha

Kadri nilivyolizoea game ndivyo na milango ya mafanikio ilivyozidi kufunguka

Nikawa naukumbuka ule msemo usemao kuteleza sio kuanguka..
 
Back
Top Bottom